Bungeni : Matukio Mbalimbali kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Thursday, 2 February 2017

demo-image

Bungeni : Matukio Mbalimbali kuhusu Wizara ya Fedha na Mipango


IMG_5656
Waziri wa Fedha na Mipango, mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akifafanua baadhi ya vipengele vya Muswada wa marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, kuhusu marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana. Muswada huo ulipitishwa kuwa Sheria na Bunge Februari Mosi, 2017.
IMG_5719
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Masaju, akihitimisha mjadala wa Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na wabunge kuwa Sheria Februari Mosi, 2017, Mjini Dodoma
IMG_5721
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Naibu Waziri wake, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), wakipitia nyaraka za Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, Bungeni Mjini Dodoma, Muswada ambao tayari Bunge limeupitisha kwa kishindo kuwa Sheria Februari Mosi, Mjini Dodoma.
IMG_5768
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akitoka nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma baada ya kutetea na kufafanua vipengele kadhaa vya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, husani eneo la Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana, na baadaye Muswada huo kupitishwa na Bunge ili uwe Sheria, Februari Mosi, 2017, Bungeni Mjini Dodoma.
IMG_5775
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akimweleza jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (Mb), nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma, baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, Februari Mosi, 2017.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)IMG_5781
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akimpongeza Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Wizara hiyo Bi. Suzana Mkapa, Nje ya Ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, kwa namna alivyoshirikiana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. George Masaju, kufanikisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na wabunge Februari Mosi, 2017.
IMG_5784
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Mb), akifurahia jambo na maafisa waandamizi wa masuala ya Sheria na Uchumi wa Wizara yake baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa Februari Mosi, 2017, mjini Dodoma.
IMG_5787
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa waandamizi wa masuala ya Sheria na Uchumi wa Wizara yake, nje ya ukumbi wa Bunge Mjini Dodoma, baada ya kupitishwa kwa marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, ikiwemo Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana.
IMG_5625
Maafisa Waandamizi wa masuala ya Sheria na Uchumi wakiambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Suzana Mkapa (kulia), wakiwasili kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, kusikiliza mjadala wa Bunge kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 4 ya Mwaka 2016, uliopitishwa na wabunge kuwa Sheria Februari Mosi, 2017.

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *