Teknolojia : Kipindi cha Take One cha Clouds TV kurudi hewani baada ya kifungo cha miezi 3 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


4 Jan 2017

Teknolojia : Kipindi cha Take One cha Clouds TV kurudi hewani baada ya kifungo cha miezi 3



Zamaradi Mketema

Kipindi hicho kilifungiwa kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.
Mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema ametangaza ujio wa kipindi hicho huku akiwataka mashabiki wa kipindi hicho kutoa maoni juu ya mabadiliko ya kipindi hicho.
“Tukiwa tumemaliza likizo yetu tuliyopewa na TCRA, kipindi chetu kinarudi rasmi January hii 2017 namaanisha Take One mtangazaji wako nikiwa yuleyule Zamaradi H. Mketema,” aliandika Instagram Zamaradi.
Aliongeza, “Hebu niambie katika msimu wetu mpya unatamani kuona nini kwenye kipindi!!? Unatamani irudi vipi ili kuboreshwa!!? Nini kiongezwe!? Nini kipunguzwe!? Nipe maoni yako tafadhali nami nitayafanyia kazi,”
Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yaliyorushwa August 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad