Matukio : Mwandishi wa Habari Amina Athumani Afariki Dunia - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


15 Jan 2017

Matukio : Mwandishi wa Habari Amina Athumani Afariki Dunia



Amina Athumani enzi za Uhai wake.


UONGOZI wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, inayochapisha magazeti ya Uhuru, Uhuru Wikiendi, Burudani na Mzalendo, unayo masikitiko makubwa kutangaza kifo cha mwandishi wake Amina Athumani.

Amina, mwandishi wa habari za michezo katika magazeti hayo, amefariki leo asubuhi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, alikokuwa amelazwa.


UONGOZI wa Kampuni ya Uhuru Publications Ltd, inayochapisha magazeti ya Uhuru, Uhuru Wikiendi, Burudani na Mzalendo, unayo masikitiko makubwa kutangaza kifo cha mwandishi wake Amina Athumani.

Amina, mwandishi wa habari za michez katika magazeti hayo, amefariki leo asubuhi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Unguja, alikokuwa amelazwa.

Amina, alilazwa kwenye hospitali hiyo baada ya kuzidiwa kutokana na kushikwa uchungu, ambapo alijifungua mtoto wa kiume, lakini kwa bahati mbaya alifariki.

Baada ya mtoto kufariki, Amina aliendelea kupatiwa matibabu hadi mauti yalipomkumba leo asubuhi.

Marehemu Amina alikwenda Zanzibar kikazi kwa ajili ya kuripoti mashindano ya Kombe la Mapinduzi, yaliyomalizika Ijumaa iliyopita. Ilikuwa arejee Dar es Salaam jana.

Mipango inafanywa na ofisi kwa ajili ya kuurejesha mwili wake Dar es Salaam leo jioni kwa boti na msiba upo nyumbani kwa ndugu wa marehemu, Kariakoo.

Mungu ilaze roho ya marehemu Amina Athumani mahala pema. Amina


Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Ndg Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athumani Ndg Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa jamaa wa marehemu katika mtaa wa kariakoo unguja leo. kutowa mkono wa pole akiwa na waandishi wa habari za michezo Zanzibar ZASWA.

Kwa taarifa za msemaji wa familia Ndg Nurdin Ramadhani amesema mwili wa marehemu tasafirishwa kesho asubuhi na Boti ya Kampuni ya Azam Marine saa moja asubuhi kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika Kijiji kwao Lushoto siku ya Jumanne mchana.

Mwili wa marehemu utawasili jijini Dar es Salaam saa tatu asubuhi ukitokea Zanzibar baada ya kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam utasafirishwa kuelekea kijiji kwao Wilaya ya Lushoto Mkoano Tanga kwa ajili ya mazishi.

Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Ndg Khamis Said akimfariji kaka wa marehemu Ndg Nurdin Ramadhani alipofika katika msiba kutowa pole leo asubuhi.

Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Said akimfariji Mume wa Marehemu Amina Athuman Ndg Toufik Majaliwa alipofika nyumbani kwa ndugu wa marehemu katika mtaa wa kariakoo zanzibar leo asubuhi kutowa mkono wa pole kwa wafiwa.





Katibu wa Kamati ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar Ndg Khamis Said akizungumza na waandishi wa habari za michezo Zanzibar Zaswa alipofika nyumbani kwa ndugu wa marehemu katika mtaa wa kariakoo zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar Ndg Mwinyimvua Mnzuki akizungumza na waandishi wa habari kwa kupokea kwa masikitiko kifo cha mwandishi mwezao mrehemu amani athuman kilichotokea leo asubuhi katika hopspitali ya mnazi mmoja.

Ndugu wa marehemu wakiwa msibari wakisubiri taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.



Wanafamilia wa marehemu Amina Athumani wakiwa katika msiba huo katika mtaa wa kariakoo Zanzibar.


Imetayarishwa na OthmanMapara.Blogspot


Zanzinews.com.


0777424152 Or 0715424152.,

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad