Matukio : Lema Amerudishwa Rumande Mpaka Februari. - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


18 Jan 2017

Matukio : Lema Amerudishwa Rumande Mpaka Februari.Mahakama ya Hakimu Mkazi Kanda ya Arusha leo imewasomea Mashtaka(Kesi ya Jinai namba 351) washtakiwa wawili ambao ni Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe.Godbless Jonathan Lema na Mke wake Neema Lema shauri hilo limekuja kwaajili yakusomwa.

Watuhumiwa hao wawili wanashtakiwa kwa kusambaza ujumbe usiofaa kwa Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kwenye simu yake ya mkoni,Mkuu wa Mkoa huyo alitumiwa meseji fupi(SMS) Inayosema "KARIBU TUTAKUZIBITI KAMA ARABUNI WANAVYODHIBITI MASHOGA" Washtakiwa wote wawili wamekana shtaka hilo,wakili wa Serikali Alice Mtenga alieleza kuwa "Ujumbe huo mfupi ulikua na nia ya kumuudhi na kumuumiza kiakili Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha"
Vilevile Upande wa Serikali wana Mashahidi watano ambao ni:

1.Mrisho Gambo

2.Joji Katabazi

3.Asp Damasi Masawe

4.Vodacom

5.Forencic Bureau na vielelezo vyao ni Print out ya vodacom simu ya mshtakiwa no 2,report ya uchunguzi kutoka Forensic Bureau.
Sambamba na hayo Jopo la Mawakili wa Mhe.Mbunge na Mkewe linalowakilishwa na wakili Msomi John Mallya(Difensive Counsel) wametoa Notisi ya Mdomo (Oral Submission) kuhusu mashtaka waliyosomewa washtakiwa hao na kuiomba Mahakama itupilie mbali kesi hiyo.

Hivyo basi Hakimu wa Mahakama hiyo Mhe.Nestory Baro Ameairisha Kesi hiyo hadi tarehe 03.02.2017 siku ya Ijumaa.
Mbunge huyo wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe.Godbless Lema alisomewa Kesi nyingine yakuhamasisha Maandamano Kesi namba 352,wakili Msomi Mallya alisema "Kwamujibu wa Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 46 ya katiba inasema Vyama vya siasa vinaruhusiwa kuandamana na kufanya Mikutano ya hadhara" baada ya wakili huyo kuwasilisha hoja zake kwa kirefu sana wakili wa Serikali Alice Mtenga Alizijibu hoja hizo na kuomba Mahakama impe muda wa ziada wakufanya submission ili aweze kujibu vizuri lakini Hakimu wa Mahakama hiyo Mhe.Bernad Nganga alisema "Sitoi muda wa ziada kwasababu ulishasimama na kujibu hoja"

Upande wa serikali walikuja na shaihidi mmoja anayefahamika kwajina la Joji Katabazi hata hivyo jopo la Mawakili wa Utetezi (Difensive Counsel)walisema shahidi huyo waliye kuja nae hawezi kuji hoja hizo wanaoweza ni Majaji watatu wa Mahakama ya Kikatiba,sambamba na hayo Mahakama imeelekeza Watakapo muhitaji shahidi huyo watamuita kwa sasa hawezi kuji hoja hizo.

Hivyo basi Kesi hiyo imearishwa hadi tarehe 08.02.2017 siku ya Jumatano.
Imetolewa

Tarehe 18.01.2017 na:

Afisa-Habari Kanda ya Kaskazini.

Post Top Ad