BoerBoel
Na Josephat Lukaza
Boerboel ni mbwa mwenye umbo kubwa, nguvu na mwenye kujiamini sana kutokana na umbo lake. Jina la BoerBoel limetokana na neno la Kiafrikana/Kiholanzi lenye maana ya Farm (Shamba). Neno Boel ni neno la zamani la kiafrikana/kidachi katika lugha za mbwa Wazungu wanasema slang word for dog.
Kwa hiyo neno boerboel likatafsiriwa na kuwa Farmer's dog (kwa kiswahili tunaweza kusema mbwa wa shamba). Kwahiyo basi aina hii ya mbwa Boerboel ni mbwa mwenye asili ya Afrika Kusini alitengenezwa kwaajili ya kulinda makazi na mashamba ya makaburu huko afrika Kusini.
Asili ya mbwa hawa imetokana na mchanganyiko wa mbwa wa asili wa afrika kusini na wale waliokuja nao makaburu wa kizungu, kifaransa na kidachi nchini afrika kusini.
Mnamo mwaka 1652 Jan van Riebeeck's aliwasili Cape town afrika kusini akiwa na mbwa aina ya "Bullenbijter" kwa kipindi hiko makaburu walikuwa na mbwa wenye maumbo makubwa , walio imara ambao walifanana na mbwa wa asili waliopatikana nchini Afrika Kusini.
Mnamo mwaka 1928 Kampuni ya Mgodi wa Almasi ya De Beers walinunua mbwa aina ya Bullmastiffs na kumsafirisha hadi Afrika Kusini kwaajili ya ulinzi wa Mgodi wao. Mbegu hii ikachanganywa na mbegu aina ya Boerboel.
Leo boerboel wamekuwa ni hobyy na kiwanda kwa Waafrika Kusini na sasa mbwa hawa wamekuwa wakisafirisha kutoka Afrika Kusini kwaajili ya kupelekwa Sehemu mbalimbali duniani.
Tabia za mbwa hawa ni kwamba kwanza wana maumbo makubwa (large size breed), wenye akili (intelligent), wanaojiamini (confidence), imara (stable), na mbwa hawa wana adabu yaani obidient kwa kizungu. Mbwa hawa wanaendelea kuwa mbwa wa ulinzi kwa wakulima wengi wa sasa hivi na nimaarufu sana kwa sababu hiyo katika jamii za mjini.
Boelboel ni mbwa mwenye nguvu sana kutokana na asili yake ya kuwa mbwa wa shamba na kuleta mtafaruku kwa wanyama wakubwa wa afrika walao nyama kama vile Simba na moja ya sababu ni kwamba wanauwezo mkubwa wa kuwalinda makaburu na watu wengine.
Mbwa hawa wanapofugwa wanapaswa kuwa na uangalizi wa hali ya juu sana na kutokana na asili yake ya ukali, inashauriwa mbwa hawa kufundishwa mafunzo ya adabu na ukali kwasababu endapo utamuacha na asiwe mkali basi mbwa huyu anaweza kuwa na ukali wa asili ambao unaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii kama kuua,Na sheria ya Nchini Kwetu Tanzania endapo Mbwa ataweza kusababisha kifo au kuua kabisa basi sharti mbwa huyo anatakiwa kuuliwa na ikumbukwe mbwa huyu ni mbwa ghali sana ambapo bei yake hufikia mpaka Randi laki 2 ambazo ni sawa na Shilingi za Kitanzania zaidi ya Milioni 29.
Angalizo: Mbwa huyu anapotaka kuvamia ni lazima akurukie kwanza shingo kwaajili ya kuweza kukudondosha chini na mara anapokurukia huwezi kumzuia kwasababu ni mbwa mwenye nguvu sana na akikuvamia ni lazima akuue kama hutopata msaada wa haraka kutoka kwa watu wengine
Huyu ndio Boerboel...Unaweza kunifuata kwenye instagram kwa jina @lukazablog facebook Josephat lukaza na Kwa Upatikanaji wa Mbwa hawa na wengine, Mawazo, Ushauri wasiliana nami kwa Simu namba 0712 390 200 au josephat.lukaza@gmail.com
No comments:
Post a Comment