Michezo : Azam Fc Yaibamiza Yanga Bao 4 - 0 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 8 January 2017

demo-image

Michezo : Azam Fc Yaibamiza Yanga Bao 4 - 0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Timu ya Azam Fc imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kwa kuipa kipigo cha mbwa mwizi cha bao 4-0 timu ya Yanga huku wakikalia usukani mwa kundi B katika kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar usiku huu.


Mpira ulianza kwa kasi ikionekana Azam FC wamepania kupata bao la mapema Dakika ya kwanza ya mchezo na katika dakika ya 2 Azam wanapata bao kupitia kwa mfungaji wao John Bocco baada ya kutokuwa na maelewano baina ya mabeki wa Yanga kwenye kuuokoa mpira uliookolewa na golikipa wa Yanga, Deogratius Munish "Dida".



Katika dakika ya 9 Yanga wanafanya shambulizi langoni mwa Azam lakini Saimon Msuva anashindwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na mrundi Amisi Tambwe.



Baada ya kuonekana kutokuwa na maelewano katika safu ya ushambuliaji Kocha George Lwandamina anafanya mabadiliko kwa kumtoa Juma Mahadhi na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin katika dakika ya 36. Mpaka Mapumziko Azam 1 Yanga 0.




Kipindi cha pili kinaanza kwa kila mmoja kumsoma mwenzake lakini katika dakika ya 54, Yahaya Mohamed anaipatia Azam goli la pili baada ya kuunganisha krosi safi Abubakar Salum " Sure Boy".



Wakiwa bado hawaamini Dk 81, Joseph Mahundi anaiandikia Azam goli la tatu baada ya kuachia shuti kali nje ya 18 na kuacha mashabiki wa Yanga wakiduwaa wakiwa hawaamini wanachokiona.



Dk 84, Atta aliyeingia kipindi cha pili anaifungia timu yake bao safi akiunganisha pasi ya Afful baada ya Mwashiuya kuukosa mpira, na mpaka mpira unamalizika Azam wanatoka kifua mbele wakiwa na alama 7 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 6.



Timu hizi zinasubiri washindi wa mechi za kesho kwenye kundi A ili kupambana nazo kwenye hatua ya nusu fainali.
IMG_9424
Kikosi cha Yanga kilichopambana usiku huu. IMG_9448


Kikosi cha Azam kilichopambana usiku huu.
IMG_9244
IMG_9299
IMG_9303
Wachezaji wakiwa wanafanya mazoezi kabla ya mechi.
IMG_9356
Timu zikiingia uwanjani wakati wa mchezo wa hatua ya makundi kati ya Yanga na Azam
IMG_9464
Saimon Msuva akimtoka beki wa Azam wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa kombe la Mpoinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.
IMG_9479
Juma Mahadhi akipambana katikati ya mabeki wa Azam wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa kombe la Mpoinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.
IMG_9517


IMG_9617
Frank Domayo (kushoto) akipambana na kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima wakati wa mchezo wa Azam na Yanga uliomalizika kwa Azam kushinda 4-0.
IMG_9661
Wachezaji wa Azam wakishangilian moja ya goli lilofungwa katika mchezo huo leo usiku.
IMG_9729
Kiungo wa Yanga Justine Zulu akiwa amebebwa na golikipa wa Yanga Ally Mustafa 'Batez' baada ya kuumia wakati wa mchezo huo na kutolewa nje.

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *