Michezo /Riadha : Gidabuday Ashinda Ukatibu Mkuu wa Shirikisho la Chama cha Riadha Nchini (RT) - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


28 Nov 2016

Michezo /Riadha : Gidabuday Ashinda Ukatibu Mkuu wa Shirikisho la Chama cha Riadha Nchini (RT)

Nikiwa na Katibu Mkuu Mpya wa Shirikisho la Chama cha Riadha Nchini, Bw. Wilhelm Francis Gidabuday, Jijini Arusha hivi karibuni . Picha/Maktaba

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Riadha Tanzania (RT), Meta Petro (kulia) na Katibu Mkuu wa Kamati ya Utendaji ya TOC,, ambaye pia mjumbe wa RT, Filbert Bayi wakipiga kura  kwenye Uwanja wa Taifa.


Na Mwandishi Wetu
UCHAGUZI Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania umefanyika leo kukishuhudia mwanariadha wa zamani, Wilhelm Gidabuday akirithi mikoba ya Katibu Mkuu wa zamani Suleiman Nyambui aliyeko nchini Brunei.
Nyambui kwa sasa ndiye kocha mkuu wa timu ya taifa ya riadha ya Brunei.
Aidha katika uchaguzi huo Anthony Mtaka aliitetea nafasi yake ya Urais wa shirikisho hilo kwa mara nyingine tena kwa kura 73 kati ya kura 74.
Gidabuday alipata kura 38 akiwapita Michael Washa (24) na Gidamis Shahanga (11) huku kura moja ikiharibika katika nafasi hiyo.
Katika nafasi nyingine, William Kalaghe alichukua nafasi ya Makamu wa Rais Utawala kwa kura 59 dhidi ya 15 zilizokwenda kwa Zainab Mbilo huku Dk. Ahmed Ndee alichukua nafasi ya Makamu wa Rais Ufundi kwa kura 74 dhidi ya kura nne za hapana.
Ombeni Zavalla aliyekuwa akikaimu Katibu Mkuu wa RT katika uchaguzi huo alipita bila kupingwa katika nafasi ya Katibu Mkuu Msaidizi kwa kura zote 74 na Gabriel Liginyani akipata nafasi ya Mweka  Hazina wa shirikisho hilo kwa kura 69 kati ya 74. 
Wengine waliopata nafasi ya Ujumbe wa RT ni Lwiza John, Meta Petro, Robert Kalyahe, Dk. Nassoro Matuzya, Rehema Killo, Zakaria Barie, Mwinga Mwanjala, Tullo Chambo, Christian Matembo na Yohana Misese.
Katibu Mkuu wa BMT afunguka 
Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja aliweka bayana  RT ndio chama pekee cha michezo nchini kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa, kwetu sisi (BMT) ni utajiri, hii ni dalili nzurihivyo ukiboronga unapoteza nafasi zote mbili, na kuongeza
Migogoro kwenye vyama inakimbiza wawekezaji na wafadhili, sio vema pindi mambo ya ndani yanapokuwa hayaendi sawasawa kukimbilia kwenye vyombo vya habari, alisema Kiganja.
Gidabuday asutwa, ajitetea
Mjumbe wa BMT na Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa na Usuluhishi ya baraza hilo Jamal Lwambo alimsuta Gidabuday kwa kauli zake ngumu alizowahi kuzitoa awali.
Katibu Mkuu mpya uliwahi kusema kwa RT wasiporudi na medali ungefanya nini ...sasa kama ulivyokuwa ukiisuta RT ukiwa bado hujaikamata nafasi hiyo watu wamekurudisha kundini wana matumaini makubwa kwako, na kuongeza
Kipindi mlichopata ni kifupi sana..hatutarajii kuona migogoro bali tunarajia kuona timu inatengenezwa vizuri ili kuleta heshima ya Tanzania, alisema Lwambo.
Kwa upande wake Gidabuday alisema, Challenge zangu kwa RT nilipokuwa nje ya shirikisho ndizo zilizonifanya nigombee nafasi hii lakini nawashukuru sana RT kwani hawakunijengea chuki kwa kuwakosoa bali walinitazama kwa upande wa uzuri.
Aliongeza, Kwa umbo mimi ni mwembamba natoa ahadi tena kama ukiniona mwakani wakati kama huu nina kitambi basi uje uniulize kulikoni, alisema Gidabuday.
Tullo Chambo atetea nafasi yake
Afisa Habari wa RT na mjumbe wa shirikisho hilo Tullo Chambo alisema, Kwa kweli kinyanganyiro mwaka huu kilikuwa kigumu ukilinganisha na msimu uliopita wakati tukiingia, lakini naamini uongozi huu kwa mara nyingine utajitahidi kufanya makubwa kuinua riadha.

AHADI ZA GIDABUDAY KABLA YA UCHAGUZI OCTOBA 11, 2016

Mwanaharakati wa Michezo, Bw . Wilhelm Gidabuday.-Ntagombea sababu ni haki yangu kikatiba katika uchaguzi ujao.

-Kwa sababu uwezo wa kuwa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo ninao na kuna mifano hai ya ushirikiano nilioutoa pale nilipohitajika kufanya hivyo.

-Nitagombea iwapo Katiba halali iliyopata baraka za BMT itatumika katika uchaguzi ujao, kama katiba haitatumika sintagombea.

-Nikiwa na bahati ya kuchaguliwa nitatumia muongozo wa KATIBA na sheria za Baraza la Micheo, ama waraka wowote utakaothibitishwa na BMT au na Wizara inayohusiana na Michezo bila kuvunja sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

ILANI / MANIFEST;

-Nitajenga upya uthibiti na matumizi stahiki ya fedha za chama (Financial Discipline) ili chama kisiwe omba omba.

-Nitashawishi ujenzi wa ofisi ya chama badala ya kuomba omba pango la ofisi.

-Nitafanya kazi ya ziada kwa kushirikiana na wadhamini wa ndani na wa nje ili kujenga KAMBI YA KUDUMU ya mazoezi ili tuepuke aibu ya kutegemea Hostels ama Hoteli ambazo sharti zilipiwe kwa fedha nyingi.

-Nitakuwa namba moja kupinga kambi za nje ya nchi, mfano ile kambi ya Timu ya Madola ya 2014 pesa nyingi zilitumika kusafirisha wanariadha kwa ndege! Zile hela za serikali ziliifaidisha EMIRATE AIRLINES, badala yake ile hela ingeweza kujenga kambi ya kudumu.

-Nitahakikisha timu zinajiandaa vyema kabla ya kukabidhiwa bendera, na nitapinga timu kuchaguliwa MEZANI ama  kwa UPENDELEO! Atakayeenda ni yule aliyeshinda kwa mujibu wa Katiba na sheria za BMT.

-Nitajenga ushirikiano wa kimataifa (Sports Diplomacy na Athletics Tourism) ili kusaidiana na sekta ya Utalii kutangaza vivutio vyetu.

-Tanzania lazima ishiriki michezo yote ya kimataifa, hapatakuwa na VISINGIZIO maana fedha tutakuwa tunazisaka kwa hali na mali, na performance lazima iwe kipimo cha faida ya fedha ipatikanayo.

-Nitahakikisha RT inajipatia miradi endelevu ili tujenge "Sustainability" tuweze kujitawala wenyewe kifedha.

-Nitahakikisha viongozi wa mikoa yote Tanzania wanapokezana safari za nje badala ya mfumo HOVYO wa sasa wa kuwa na "Special Frequent Travelers" ni lazima kila kiongozi kutoka mikoa yote wapate nafasi ya "Exposure" ili warudi kujenga riadha katika mikoa yao.

-Nitahakikisha HAKI STAHIKI za wanariadha zinalindwa, kama vile CONTRACT ZA KAMPUNI ZA VIATU, MATANGAZO na BIMA ZAO ZA AFYA.

-Nikishindwa kwa mujibu wa Katiba nitafurahi na nitampongeza aliyeshinda.

-Nikishinda SINTAPAGAWA, bali nitamshukuru MUNGU na kuanza kazi ya kujenga riadha yetu.

-Kazi ya kwanza ni kuimarisha OFISI na miundombinu ya KAMBI alafu ROAD TO 2020 TOKYO OLYMPIC GAMES.

ILE FIKRA POTOFU NA YA KIFISADI ILIYOOTA MIZIZI KTK VYAMA VYA MICHEZO YA KUWEKANA MADARAKANI KINDUGU, KIKANDA NA KIRAFIKI HAINA NAFASI TENA.

By Gidabuday,
October 11th 2016.

Post Top Ad