Matukio : Waziri Mkuu, Majaliwa aongoza wabunge kuaga mwili wa Mbunge wa Dimani - Hafidh Hally Tahir - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Friday, 11 November 2016

Matukio : Waziri Mkuu, Majaliwa aongoza wabunge kuaga mwili wa Mbunge wa Dimani - Hafidh Hally Tahir



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa pamoja na wabunge wakiwa wamesimama kimya kwa dakikika moja kwa heshima ya mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. Hafidh alifariki dunia usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Mbunge wa Dimai Hafidh Ally Tahir, bungeni mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Spika wa Bunge, Job Ndugai akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoa heshima za mwisho kwa mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Novemba 11, 2016. Mbunge huyo alifariki dunia mjijini Dodoma usiku wa kuamkia leo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama (wapili kulia) na Katibu wa Bunge, Dkt.Thomas Kashililah wakisubiri kupokea mwili wa Mbunge wa Dimani, marehemu Hafidh Ally Tahir kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma ambako ulisafirishwa kwenda Zanzibar kwa Mazishi Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai na Kiongozi wa  Upinzania bungeni, Freeman Mbowe (kulia) wakishuhudia wakati mwili wa mbunge wa Dimani, Hafidh Ally Tahir ukipandishwa kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Dodoma ili kusafirishwe kwenda Zanzibar kwa mazishi Novemba 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameongoza wabunge kuuaga mwili wa aliyekuwa mbunge wa Dimani, Zanzibar Mheshimiwa Hafidh Ally Tahir.

Bw. Tahir amefariki saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na mwili wake kuagwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kwa mazishi.

Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia ya marehemu na wabunge wote.“Tumepokea taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Leo tupo katika wakati mgumu sana. Tumeondokewa na viongozi wengi,” amesema.

Amesema wafiwa wanatakiwa kuishi kwa upendo. “Tumuombee marehemu, tuiombee familia iwe na moyo wa utulivu katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.”

Bw. Hafidh alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta.Enzi ya uhai wake, alishiriki kikamilifu katika masuala ya michezo; alikuwa mwamuzi wa soka mwenye beji ya FIFA na kocha msaidiizi wa timu ya soka ya Bunge.

Hadi jana, Bw. Hafidh alishiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa kupata viongozi wa Tawi la Umoja wa Wabunge WanaYanga mjini Dodoma ambapo yeye alichaguliwa kuwa Katibu.




IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, NOVEMBA 11, 2016.

No comments:

Post a Comment