Michezo : Yanga yaibamiza Ruvu shooting 2 - 1, uwanja wa Uhuru - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


11 Nov 2016

Michezo : Yanga yaibamiza Ruvu shooting 2 - 1, uwanja wa Uhuru

MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, Yanga leo wameendeleza ubabe wao baada ya kuwadidimiza Maafande wa Ruvu Shooting goli 2-1 na kufikia alama 33 nyuma ya mahasimu wao Simba wenye alama 35.

Dakika ya 6 ya mchezo, Ruvu walianza kufungua pazia la magoli kupitia kwa mshambuliaji wake Abraham Mussa baada ya kufanya shambulio la kushtukiza langoni kwa Yanga.

Yanga walianza kulisakama lango la Ruvu shooting na katika dakika ya 32, Simon Msuva akaisawazishia timu yake goli na kufanya matokeo kuwa 1-1 mpaka mapumziko.

Kabla ya kipindi cha pili kuanza kocha wa Yanga, Hans Van De Pluijm anatolewa nje kwa amri ya mwamuzi wa mchezo huo, Mathew Akram kutoka jijini Mwanza baada ya kumzonga na kwenda kushuhudia kipindi cha pili cha mchezo huo akiwa jukwaani na mashabiki.

Ukiwa umeanza kwa kasi kwa kila upande kutafuta goli la kuongoza na katika dakika ya 56 juhudi za Donald Ngoma zinaisaidia Yanga ambapo Haruna Niyonzima anaachia shuti kali lililotinga kimiani na kuiandikia Yanga goli 2.

Kila upande wakiwa wanashambuliana kwa zamu mpaka dakika 90 zinamalizika Yanga anatoka kifua mbele kwa ushindi wa goli 2-1.
Mshambuliaji wa Yanga, Simon Msuva akiiandikia timu yake bao la kusawazisha katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara, uliopogwa katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam leo. Yanga imeshinda bao 2-1.
Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Thaban Kamusoko akichuana vikali na Beki wa Ruvu Shooting, Shaibu Nayopa, wakati wa Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es salaam leo. Yanga imeshinda bao 2-1.


Post Top Ad