Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu
mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na historia ya mchakato huo kwa
vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Afisa
wa IRI, Tony Alfred akizungumza jambo wakakati wa mafunzo ya mchakato
wa mabadiliko ya Katiba kwa vijana wa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Makamu mwenyekiti wa TYVA, Kamala Dickson akizungumza jambo kwenye mkutano huo
Baadhi ya Vijana wa wilaya ya Chamwino wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba.
Katibu Mtendaji wa TYVA Saddam Khalfan akitoa ufafanuzi kuhusu shirika hilo wakati wa mafunzo hayo.
Baadhi ya Vijana wa wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Katiba Tanzania Bw, Deus Kibamba akitoa elimu kuhusu
mchakato wa mabadiliko ya Katiba pamoja na changamoto zake kwa vijana wa
wilaya ya Tanga Mjini mkoani Tanga.
Mmoja wa washiriki akichangia mada
Kijana
mwenye ulemavu wa ngozi akisoma katiba ya Tanzania kwa makini sana
wakati wa mafunzo kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba yaliyofanyika
Mjini Tanga.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo yaliyofanyika Tanga wakifuatilia mada
Na Mwandishi Wetu
Asasi
Ya Vijana, Tanzania Youth Vision Association kwa Kushirikiana Na
International Republican Institute zimetoa mafunzo ya kuboresha Uwezo wa
Vijana kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba nchini katika Mikoa
mitatu ilijumuisha Wilaya Nne, ikiwemo Kinondoni, Dodoma Mjini, Chamwino
Na Tanga Mjini.
Mafunzo hayo yameweza kufikia vijana 500 kwa njia ya Warsha na Vijana aa wananchi zaidi ya 100,000 kupitia mitandao ya kijamii.
Lengo
kuu la Mafunzo hayo ni kuongeza uelewa na ushiriki wa Vijana katika
mchakato wa Mabadiliko ya Katiba. Katika ufunguzi wa mafunzo hayo,
Katibu Mtendaji wa TYVA ndugu Saddam Khalfan alisema, TYVA inaamini
Katiba ni Sheria mama na mwongozo ambao una uhusiano wa moja kwa moja na
maisha yetu ya kila siku.
Alibainisha
watu wengi wamekua wakisoma au kuisikia Katiba, na wengine wakidhani
Katiba ni maalumu kwa ajili ya wanasheria au wasomi tu. Kuna uhusiano
mkubwa kati ya Katiba bora ya Nchi, Demokrasia na Maendeleo ya Jamii.
Mwanaharakati
Na Mtetezi wa HAKI za Binadamu ndugu Deus Kibamba alipata kuwaelezea
washiriki wa mafunzo hayo historia ya mchakato wa mabadiliko ya Katiba,
Ushiriki wa wananchi katika mchakato wa Katiba, hatua muhimu katika
Mchakato wa utengenezaji Katiba, Mambo ya Msingi yaliyomo katika Katiba
inayopendekezwa na Mambo muhimu kuelekea kura ya Maoni ya Katiba
Inayopendekezwa.
Alidokeza
pia, katika mchakato wa Katiba, hasa katika hatua ya Bunge la Katiba
ulikosa maridhiano ya Kitaifa. kuna haja ya kuwepo mkutano wa kitaifa
utajaowaleta wadau na jopo la wataalamu mbalimbali kwa ajili ya
kunyambua yale mambo yanayoendelea kuleta ukakasi linapaswa kufanyika.
Ndugu
Dickson Kamala ambaye ni Mtetezi wa HAKI za vijana na Makamu Mwenyekiti
Wa TYVA aliwasilisha mada ya umuhimu wa Vijana kushiriki na
kushirikiana katika mchakato wa mabadiliko ya Katiba ili kupata Katiba
itayojali maslahi yao na ya Taifa kwa ujumla.
Afisa
kutoka IRI, Tony Alfred aliwatarifu Vijana washiriki kusoma kuhusu
Katiba na wanaweza kupata habari na taarifa zaidi kuhusu Katiba kwa
kupitia ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutuma Neno "Katiba yetu" Kwenda
0684996494.
No comments:
Post a Comment