Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo
cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (kushoto) pamoja na mkuu wa chuo hicho
Prof. Innocent Ngalinda (kulia) kuingia ukumbini pamoja na wahitimu
tayari kwa mahafali.
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo
cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua mahafali ya pili
yaliofanyika chuoni hapo.
Sehemu ya Wahitimu wa Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika.
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo
cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimtunuku mmoja wa wahitimu kati
ya wahitimu 133 waliohitimu leo na kutunukiwa Shahada na Stashahada.
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo
cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi wa Sudan
Mhe.Mahgoub Ahmed Sharfi , ambapo mabalozi mbali mbali walihudhuria.
Mgeni
Rasmi katika Mahafali ya Pili ya Kutunuku Shahada na Stashahada za Chuo
cha Takwimu Mashariki ya Afrika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja
Mabalozi wa nchi mbali mbali waliohudhuria mahafali hayo.
Na Benny Mwaipaja
MAKAMU wa Rais
Mama SAMIA SULUHU HASSAN, amesema kuwa matumizi sahihi ya takwimu
zilizokusanywa kwa njia ya weledi mkubwa yanaweza kuchochea maendeleo ya
kijamii na kiuchumi kwa kasi zaidi Barani Afrika,
Mama Samia ametoa
kauli hiyo leo wakati akiwatunuku astashada na shahada wahitimu 154 kutoka nchi saba za kiafrika
ikiwemo Tanzania, wakati wa Mahafali ya Pili ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa
Afrika (EASTC) kilichoko Changanyikeni Jijini Dar es salaam.
Amewataka wahitimu
hao kutumia elimu na ujuzi walioupata katika chuo hicho kufanya utafiti rasmi
na wenye viwango ili nchi wanachama walioanzisha chuo hicho waweze kutumia
takwimu sahihi kupanga mipango yao ya maendeleo itakayosaidia kuwaondolea
umasikini wananchi wake
Pause Mhe. Samia
Suluhu Hassan-Makamu wa Rais-Tanzania
Aidha,
amewahakikishia wahitimu kutoka Tanzania waliomaliza masomo yao katika chuo
hicho kwamba serikali itawapatia ajira ili kuongeza kada ya wasomi waliohitimu
mafunzo ya takwimu rasmi ili kuchochea maendeleo ya nchi
Kwa upande wake,
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa Tanzania inatekeleza Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa Taifa ambapo moja ya mambo yatakayosaidia kufanikisha mpango huo
ni matumizi ya takwimu rasmi na sahihi na kuwataka wahitimu kutoka Tanzania
kusaidia kufanikisha nchi kuwa nchi ya viwanda.
Mkuu wa Chuo hicho
kilichoanzishwa miaka 51 iliyopita, Profesa Innocent Ngalinda, ameiomba
serikali ya Tanzania na nchi wanachama walioanzisha Taasisi hiyo ya elimu ya
juu ya Takwimu Rasmi, kuijengea uwezo ikiwemo miundombinu ya majengo pamoja na
wakufunzi ili kiweze kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu hiyo muhimu
Akitoa neno la
shukurani kwa mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Taifa Dkt.
Albina Chuwa, amesema serikali imejipanga kutumia wataalamu wa takwimu Rasmi
waliobobea walioko serikalini na katika sekta binafsi kufanikisha utafiti wa
sekta ya viwanda unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Wahitimu wa
Mahafali ya Pili katika Chuo hicho cha Takwimu Mashariki mwa Afrika wametoka
katika nchi za Nigeria, Ghana, Ethiopia, Somalia, Uganda, Liberia, Rwanda na
wenyeji Tanzania.
No comments:
Post a Comment