Michezo : Timu ya Golf ya JWTZ Lugalo yaweka Heshima katika Golf, Yanyakua Kombe la Waitara - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


20 Nov 2016

Michezo : Timu ya Golf ya JWTZ Lugalo yaweka Heshima katika Golf, Yanyakua Kombe la Waitara


Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara,kulia akibadilishana Matokeo na wachezaji wenzie,katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana (kushoto) na katibu mkuu wizara ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima katikati katika mashindano ya Waitara Trophy Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara,kulia akibadilishana Mawazo na wachezaji mwenzi ambaye ni katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Abdulrahman Kinana (katikati) katika mashindano yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam kushoto ni katibu mkuu Wizara ya ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh Job Masima.
Mshindi wa Jumla wa kombe la Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara, kutoka klabu ya Lugalo Juma likuli akiwa amenyenyua vikombe alivyokabidhiwa na Jaji Mkuu Mh Othman Chande aliyekuwa mgeni rasmi katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Klabu ya Lugalo brigedia Jenerali Michael Luwongo akiwa ameshika zawadi ya kikombe alichokabidhiwa na Chama cha Golf Tanzania TGU ikiwa ni ishara ya Kutambua Mchango wa Klabu hiyo katika kukuza mchezo wa Golf Nchini kulia ni mweka hazina wa TGU Akhil Yusuphali mara baada ya mashindano ya Waitara yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam.
Mshindi wa Kundi la Wanawake wa kombe la Mkuu wa Majeshi Mstaafu George Waitara, kutoka klabu ya Lugalo Sophia Mathias akipokea zawadi ya Meza aliyekabidhiwa na Mke wa Jenerali Mstaafu Waitara katika mashindano hayo yaliyofanyika Jumamosi Novemba 19 jijini Dar es salaam.(Picha Luteni Selemani Semunyu).

Na Luteni Selemani Semunyu

Timu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo imeweka heshima katika mchezo huo baada ya kunyakua Ubingwa wa kombe la mkuu wa majeshi Mstaafu  George Waitara kwa mara ya tatu katika mashindano yaliyochezwa Jumamosi Novemba 19 Jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mchezaji wake Juma Likuli kuibuka mshindi wa Jumla baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 66 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni Tano na kuwashinda Wachezaji  zaidi ya 100 kutoka vilabu mbali mbali nchini waliojitokeza kushiriki mashindano hayo.

Katika Divisheni A  Cloud Mtavangu wa Lugalo aliibuka na ushindi kwa Mikwaju ya Jumla 67 baada ya kupiga mikwaju 74 na kiwango chake cha Uchezaji Kikiwa ni saba na kufuatiwa na Hendrick Nyenza wa Lugalo kwa CountBack  baada ya kupiga mikwaju ya Jumla 68 huku kiwango chake cha Uchezaji Kikiwa ni Tatu.

Katika Divisheni B  Iddi Ramadhani  wa Lugalo aliibuka na Ushindi Baada ya Kupiga Mikwaju ya Jumla 67 huku kiwango chake cha Uchezaji Kikiwa ni 18 akifuataiwa na Noel Mheni wa Lugalo baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 69 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni 15.

Katika Divisheni C mpiga golf A, Ngamilo wa klabu ya Gymkhana ya Dar es Salaam aliibuka na Ushindi baada ya Kupiga Mikwaju ya Jumla 74 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni 24 akifuatiwa na Alfred Kinswaga wa Lugalo baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 75 huku kiwango chake cha Uchezaji Kikiwa ni 20.

 Kwa upande wa Senior Mpiga Golf Saidi Nkya wa Lugalo aliibuka na Ushindi baada ya kupiga Mikwaju ya Jumla 73 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni 15 akifuatiwa na Boniface Nyiti wa Lugalo aliyepiga mikwaju ya Jumla 74   huku kiwango chake cha Uchezaji  kikiwa ni Nane .

Kwa upande wa kundi la Wanawake Sophia Mathias wa Lugalo aliibuka Na ushindi baada ya Kupiga Mikwaju ya Jumla 74 huku kiwango chake cha Uchezaji kikiwa ni 13 akifuatiwa na Vicky Elias  aliyepiga Mikwaju ya Jumla 76 huku kiwango cha Uchezaji Kikiwa ni Tisa.

Kwa Upande wa Wachezaji wa kulipwa Nuru Mollel wa Klabu ya Gymkhana ya Arusha aliibuka na ushindi na katika kundi la Wachezaji wasaidizi  Robert Jamson aliibuna na Ushindi kwa Mikwaju ya Jumla 65 akifuatiwa na Gerad Gadiel.

Hili linakuwa kombe la pili kuchukuliwa moja kwa moja na klabu ya Lugalo baada ya kutimiza vigezo vya kulinyakua mara tatu mfululizo baada ya pia Kombe la mkuu wa majeshi CDF TROPHY  ambalo nalo sasa limeenda moja kwa moja kwa Lugalo na mwakani inapaswa kutafutwa makombe mapya.

Post Top Ad