Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza ziara yake ya siku 10
ndani ya jiji la Dar es salaam kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi
pamoja na kuzitafutia ufumbuzi.
Ziara
hiyo imeanzia katika wilaya ya Kigamboni ambapo kabla ya kwenda
kusikiliza kero za wananchi mtaani, Mkuu huyo alizungumza na viongozi wa
wilaya hiyo pamoja na kuzindua mpango mkakati wa mkuu wa wilaya ya
Kigamboni.
Akiongea na viongozi hao wa wilaya ya Kigamboni, Makonda amesema anafanya ziara hiyo ili kugundua kero za wananachi pamoja kuwahamasisha wafanyakazi wa serikali kuwajibika."Nataka wafanyakazi wafanyekazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Rais wetu, nimegundua asilimia 80 ya wafanyakazi wa serikali hawafanyi kazi, asilimia 80 ya watumishi umma hawafanyi kazi, ni wapiga majungu, wasoma magazeti, niwambea. Kilichobaki ni kusubiri mwisho wa mwezi kwa ajili ya mshahara," alisema Mkonda.
Pia Makonda alisema hataki kuona wananchi wanakimbilia kwa mkuu wa mkoa kuomba msaada wa utatuzi wa changamoto zao wakati serikali inawafanya kazi kuanzia ngazi ya vitongoji.Aidha mkuu huyo alitembelea pia mtaa wa Maweni, Mjimwema ambapo alishuhuda uharibifu mkubwa wa mazingira na kumtaka mkuu wa wilaya hiyo pamoja na vyombo vya ulinzi kuwashghulikia wote watakaoendelea kuchimba kokoto eneo hilo.

wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizindua mpango kazi wa manispaa
ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam. Katika ni Mkuu wa Wilaya ya
Kigamboni,Hashim Mgandilwa na kulia ni Mkurungenzi wa manispaa ya
Kigamboni,Stepheni Katembe.
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akizungumza machache katika
uzindunzi wa mpango kazi wa manispaa ya Kigamboni leo jijini Dar es
Salaam.
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda na Kamisha wa Polisi Simon Sirro,
wakimuangalia mmoja wa vijana wa kituo cha kuwasaidia vijana
waliothirika na dawa za kulevya cha PEDEREF Sober,Kigamboni ambaye
alikuwa akitia ushahidi wa jinsi alivyoathiriwa na dawa hizo kwa kubeba
dawa tumboni, wakati wa ziara ya mkuu huyo wa mkoa, wilayani humo,leo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikagua uharibifu wa mazingira
machimbo ya kokoto Mjimwema jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa
Wilaya ya Kigamboni,Hashim Mgandilwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akikagua machimbo ya kokoto yalipo Mjimwema jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na vijana wa Sober House iliyopo Vijibweni leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro
akiwa katika picha ya pamoja na vijana kutoka asasi mbalimbali zisizo za
kiserikali zinazo jitolea kusikiliza changamoto na kero za wananchi
wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akipokea zawadi kutoka kwa Mmiliki wa Kituo cha vijana wa Sober House,Nuru Saleh leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akipokea zawadi kutoka kwa Mmiliki wa Kituo cha vijana wa Sober House, Nuru Saleh leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
No comments:
Post a Comment