Katibu
Tawala Msaidizi, kitengo cha elimu mkoani Mwanza, Khamis Maulid,
akifungua warsha ya mafunzo ya filamu ya siku tatu mkoani Mwanza
iliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini kwa ajili ya Wasanii wa Filamu
mkoani Mwanza.
Na BMG
Maulid
amesisitiza wasanii hao kuhakikisha wanatengeneza filamu zenye ubora na
zinazozingatia maadili ya mtanzania na kukaguliwa kabla ya kuingia
sokoni hatua ambayo itasaidia kukuza soko la filamu mkoani Mwanza.
Pamoja
na mambo mengine, warsha hiyo imelenga kuwawawezesha kielimu wasanii wa
filamu mkoani Mwanza kutengeneza filamu zenye ubora, namna ya uanzishwa
wa vikundi na kampuni za filamu, uandishi wa miswada ya filamu,uongozi
wa filamu pamoja na taaluma ya upigaji picha.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo, akielezea majukumu ya
bodi hiyo ambayo ni pamoja na kuhakikisha ubora wa filamu pamoja na
hakimili za wasanii wa filamu nchini.
Wasanii
wa filamu mkoani Mwanza wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
nchini, Joyce Fissoo, wakati wa warsha kwa wasanii hao hii leo.
Afisa
Uendeshaji na Maso kokutoka Mfuko wa Pensheni PPF akielezea umuhimu wa
wasanii wa filamu mkoani Mwanza kujiunga na mfuko huo ili kunufaika na
mafao kutokana na kazi zao za sanaa.
PPF ni
miongoni mwa wadau waliosaidia kufanikisha warsha ya mafunzo kwa
wasanii wa filamu mkoani Mwanza yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
Kutoka
kushoto ni Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba,
Katibu Tawala Msaidizi, kitengo cha elimu mkoani Mwanza, Khamis Maulid
pamoja na afisa kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Mjumbe
wa Bodi ya Filamu Taifa kutoka mkoani Mwanza, Hussein Kimu (katikati)
akiwa pamoja na wajumbe wengine wa bodi hiyo pamoja na wasanii wa Filamu
mkoani Mwanza.
Zaidi ya wasanii 300 wa Filamu mkoani Mwanza wakifuatilia warsha ya mafunzo ya filamu yaliyoandaliwa na Bodi ya Filamu nchini.
Rais
wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, amesema mkoani
Mwanza kuna fursa nyingi kwenye soko la filamu ikiwemo mandhari nzuri
hiyo wasanii wa filamu mkoani Mwanza watumie fursa hiyo kuboresha soko
lao la filamu.
Mjumbe
wa Bodi ya Filamu Taifa kutoka mkoani Mwanza, Hussein Kimu, amesema
mafunzo hayo yatawasaidia wasanii wa Filamu mkoani Mwanza katika
kuboresha filamu zao na hivyo kuinua soko la Filamu mkoani Mwanza badala
ya kutegemea soko hilo Jijini Dar es salam pekee.
Baadhi ya wasanii wa Filamu mkoani Mwanza wakipiga picha na viongozi Filamu nchini.
Mmoja
wa wasanii wa Filamu mkoani Mwanza (kushoto) akisalimiana na Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo (katikati), kulia ni
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba.
Mmoja
wa wasanii wa Filamu mkoani Mwanza (kushoto) akisalimiana na Rais wa
Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba, katikati ni Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo
Viongozi
mbalimbali, akiwemo Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon
Mwakifwamba (wa kwanza kushoto), Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
nchini, Joyce Fissoo (wa pili kushoto) pamoja na Innocent Mungy kutoka
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA (wa kwanza kulia).
Baadhi ya wasanii wa Filamu mkoani Mwanza wakipiga picha na viongozi Filamu nchini.
Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment