Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Milade Nabii Sheikh Sheraly Shamsi akifafanua jambo wakati Kamati yake ilipofika kwa Balozi Seif kumualika ushiriki wa sherehe za Maulidi ya Uzawa wa Mtume Muhammad |
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Sherehe
za Maulidi ya Uzawa wa Kiongozi wa Dini ya Kiislamu Ulimwenguni Mtume
Muhammad {SWA } Kitaifa zinatarajiwa kufanyika Mnamo Mwezi 11 Mfunguo
Sita kutegemea kuandama kwa Mwezi sawa na Tarehe 11 Disemba mwaka huu wa
2016.
Mwenyekiti
wa Kamati Tendaji ya Jumuiya ya Milade Nabii Zanzibar Sheikh Sheraly
Shamsi alieleza hayo wakati akiuongoza Ujumbe Wanne wa Viongozi wa
Kamati hiyo kutoa mualiko wa Maulidi hayo kwa Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Seikh
Sheraly Shamsi alimueleza Balozi Seif kwamba yapo mabadiliko kidogo
katika maandalizi ya Maulidi kwa upande wa washiriki wa mwaka huu
uliotoa fursa pana zaidi katika ushiriki wa madrasa katika kupata Qasida
mchanganyiko pamoja na wasomaji wa Tajwid kutoka Wilaya zote za Unguja
na Pemba.
Alisema
Wajumbe wa Kamati Tendaji ya Milade Nabii walipata kazi kubwa katika
kufanya mchujo wa Vijana walioandaliwa kushiriki kwenye Maulid hayo
katika usomaji wa Tajwid na Qasida kazi iliyoanza tokea mwezi mfungo wa
Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Hata
hivyo Mwenyekiti huyo wa Kamati tendaji ya Milade Nabii alisema yapo
malalamiko yaliyojitokeza kwa baadhi ya washiriki wa maandalizi hayo,
lakini wajumbe wa Kamati yake muda wote walikuwa makini katika kufanya
mchujo huo uliokwenda kwa kuzingatia haki ya kila mshiriki.
Sheikh
Sheraly alimuhakikisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba
maandalizi ya sherehe hizo yameanza kwa mafanikio makubwa na washiriki
wa maulidi hayo katika makundi ya Madrasa na wanafunzi wa Tajwid kutoka
Kisiwani Pemba wamepangiwa utaratibu maalum wa kuwasili Unguja.
Naye
Mjumbe wa Kamati hiyo Sheikh Kassim Haidar Jabir aliishukuru na
kuipongeza Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kupitia Idara
yake ya Sherehe na Mapambo kwa msaada mkubwa inayotoa katika kufanikisha
Sherehe hizo muhimu.
Sheikh
Haidar alisema Idara ya Sherehe na Mapambo ni mshirika mkuu wa Kamati
Tendaji ya Milade Nabii jambo ambalo uungaji wake mkono umekuwa
ukiirahisishia kazi Kamtio hiyo katika maandalizi ya kufanyika kwa
Maulidi hayo ifikapo Mfunguo Sita ya Kila mwaka.
Akitoa
shukrani zake kwa mualiko wa Maulidi hayo ya Mwaka huu Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliipongeza Kamati Tendaji hiyo pamoja
na Waumini wote wa Dini ya Kiislamu Nchini kwa jitihada wanazoendelea
kuchukuwa za kufanikisha sherehe hizo.
Balozi
Seif alisema Jamii imekuwa ikishuhudia harakari za maandilizi ya
sherehe hizo zikiendelea katika maeneo mbali mbali Nchini bila ya
kutokea hitilafu zozote tokea kuanza kwake miaka mingi iliyopita.
Sherehe
za Maulidi ya uzawa wa Mtume Muhammad {SAW } Kitaifa zimekuwa
zikifanyika ifikapo Mwezi 11 Mfunguo Sita ya Kila mwaka hapa Nchini na
kushirikisha Waumini wa Dini ya Kiislamu kutoka sehemu mbali mbali ya
Visiwa hivi na nje ya Zanzibar.
No comments:
Post a Comment