Askari
wa usalama barabarani Koplo Athilio Choga akitoa maelezo mafupi ya
barabara zilizopo mkoani Arusha na jinsi magari yanavyoingia na kutoka
katika siku ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyoanza leo 7 - 11
katika viwanja vya sheikh Amri Abeid ,mbele ni mkuu wa wilaya ya
Arusha Gabriel Fabian Daqarro ambapo alikuwa mgeni rasmi
Askari polisi wa kikosi cha usalama
barabarani CPL Abdallah Mkumba akimuonyesha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Arusha
jinsi kifaa chakupimia ulevi kwa madereva kinavyo fanya kazi , kulia ni Balozi CPL Ismael Katenya.
Kabla ya sherehe kuanza kulikuwa na
maaandamano kwa askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwasili
katika viwanja vya sheikh Amri Abeid kwa maandamano
Kikundi cha walemavu wao pia walijitokeza katika sherehe hizi za uzinduzi wa siku ya Nenda kwa usalama barabarani
Kikundi cha ngoma cha wanafunzi nacho kilikuwepo katika sherehe hizi za siku ya usalama barabarani
Wageni waalikwa wakiwa wanafuatilia uzinduzi huo leo katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid
Mlezi wa RSA -Arusha na Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani SSP Eng. Nuru Selemani akisoma risala kwa Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel F. Daqarro.
Hata
hivyo ajali hizo za pikipiki kwa mwaka 2010 zilikuwa 709 ukilinganisha
na ajali 277 za pikipiki mwaka 2009 ajali hizo za pikipiki bado
zinaendelea kuongezeka.
Hayo
yamebainishwa na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Arusha SSP. Eng. Nuru Selemani
wakati akielezea hali ya usalama wa barabarani kwenye uzinduzi wa
maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mapema leo
Selemani
alisema kuwa takwimu zinaonesha mkoa wa Arusha bado unakabiliwa na
ajali za barabarani ambapo kwa kipindi cha mwaka 2007 ajali zimekuwa
zikiongezeka na kulikuwa na ajali 1807 na kufikia kiwango cha juu mwaka
2010 ambapo ajali 2658 huku kwa kipindi cha mwaka 2012 ajali zilianza
kupungua hadi kufikia ajali 2011
Alifafanua
kuwa baada ya jeshi kutumia nguvu kubwa sana katika kupunguza ajali
zinazotokana na magari zilipungua sana ingawaje kwa sasa bado wimbi
kubwa la ajali linatokana na ajali za pikipiki.
Katika
hatua nyingine alisema kuwa ajali zinasababishwa na sababu za
kibinadamu kwa asilimia 75,madereva kulewa huku wakiwa wanaendesha
vyombo vya moto,pia ubovu wa vyombo vya usafiri kwa asilimia
15,miundombinu ya barabara kwa asilimia10.
Awali
mgeni rasmi katika uzinduzi huo mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Fabian Daqaro
alisema jukumu la usalama wa barabarani sio la polisi wenyewe wala
kamati ya kikosi cha usalama barabarani pekee bali ni ulinzi wa kila
mtu.
Fabian
alisema kuwa endapo kama kila mtu atafuata sheria na kanuni za
barabarani basi ajali zitakuwepo kwa kiwango cha asilimia 0.0 kwani
ajali zinachangia kudidimiza mlengo wa taifa.
Hata hivyo
katika uzinduzi huo baadhi ya askari wa usalama barabarani walifanikiwa
kupewa vyeti vya ufanyakazi bora ambapo mmoja wa askari hao Silas Konga
alisema kuwa maadili yao bora kazini yamechangia wao kutambulika na
jeshi hilo.
No comments:
Post a Comment