Taasisi
ya Tanzania Yemeni Professional Foundation (TYPF), Jumamosi ya Novemba 5
mwaka huu iliendesha huduma ya upimaji wa afya kwa akina mama wa Mkoa
wa Dar es Salaam kwa udhamini wa Ofisi ya Ubalozi wa Kuwait nchini
Tanzania.
Shughuli
iliyopewa jina la Women’s Health Day, ilikuwa na lengo la taasisi hiyo
kutoa huduma bora kwa akina mama kama sehemu ya kuangalia namna ya
kusogeza huduma karibu na wananchi sambamba na kuhamasisha suala zima la
upimaji wa afya ya akina mama.
Akizungumza
katika shughuli hiyo ya upimaji afya kwa wanawake, Mwenyekiti wa
Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), Dr Ameir Binzoo, alisema
huduma hiyo ya upimaji afya ilikuwa na dhamira ya kuwasaidia akina mama
kufahamu afya zao.
Alisema
Siku hiyo ya afya ya wanawake ilidhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait, ikiwa
ni hatua bora ya kushirikiana na wadau wa afya kuwasaidia wanawake wote
wa jijini Dar es Salaam, wakiwamo wale waliohudhuria katika upimaji huo.
“Tunashukuru
kwa kufanikiwa kumaliza salama tukio letu kwa sababu limefanyika vizuri
na kusudio letu tulilotaka limefika kwa wahusika, wakiwamo akina mama
wa jijini Dar es Salaam ambao ndio walengwa haswa.
“Tunawapongeza
pia wenzetu wa Ubalozi wa Kuwait kwa kuguswa kwenye suala la afya ya
wanawake hali iliyowasukuma kuingia kwenye tukio letu la kutoa huduma ya
bure ya afya ya wanawake,” alisema Dr Binzoo.
Kwa
mujibu wa Dr Binzoo, mbali na kuwapima wanawake hao waliohudhuria, pia
walikuwa wakitoa elimu na mbinu ya kukabiliana na magonjwa ikiwamo
kujiwekea utaratibu wa kupima afya zao mara kwa mara.
Mwenyekiti
wa Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), Dr Ameir Binzoo
(kushoto) akimpatia zawadi Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mheshimiwa
Jasem Al Najem kwa udhamini wa siku ya afya ya mwanamke iliyoandaliwa na
taasisi hiyo nchini na kudhaminiwa na Ubalozi wa Kuwait kwa ajili ya
kuboresha afya ya mwanamke jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait akipata picha ya pamoja na wadau wa taasisi hiyo baada ya kumalizika shughuli ya upimaji afya kwa akina mama.
Balozi
wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al Najem akipewa maelekezo aliposhiriki
katika shughuli ya upimaji afya kwa wanawake jijini Dar es Salaam
iliyoandaliwa na Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF).
No comments:
Post a Comment