Urembo / Ubunifu : Warembo 16 kuwania taji la Miss Temeke 2016 - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


18 Sept 2016

Urembo / Ubunifu : Warembo 16 kuwania taji la Miss Temeke 2016


Washiriki wa Miss Temeke 2016 wakifanya mazoezi ya kujiandaa na shindano lao jijini Dar es Salaam. Shindano hilo, litakalofanyika Viwanja vya Sigara TCC Chang'ombe Septemba 24 mwaka huu.

Na Dotto Mwaibale

WAREMBO 16 wanatarajia kupanda jukwaani katika shindano la kumpata Miss Temeke 2016 litakalofanyika Septemba 24 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam  katika mazoezi yao, Mwalimu wa warembo hao Neema Honest alisema warembo wote wapo fiti na wanaendelea vizuri na mazoezi Chang'ombe Sigara TCC.

"Washiriki wote wapo katika hali nzuri na sasa wanaendelea na mazoezi tayari kwa shindano hilo litakalofanyika Chang'ombe Sigara TCC" alisema Honest.

Aliwataja warembo kuwa ni Jesca  Nassary, Diana Nyaki, Juliet Pallangyo, Irene Tomitho, Macrina Kudema, Anitha Mugisha, Khadija Masoud na Sia Kiweru.

Aliwataja wengine kuwa ni Sara Bigambo, Nancy Mushi, Mwantum, Esther Mnaki, Anitha Kisimba na Clara Premsinga.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad