Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa mafunzo
Na Oyuke Phostine
Wizara ya Fedha
na Mipango – Tume ya Mipango inatoa mafunzo kwa maafisa mipango kutoka mikoa ya
Arusha, Tanga na Kilimanjaro ili kuwawezesha kuchambua na kuchagua miradi
itakayoleta tija kwa taifa na inayoendana na Mpango wa Pili wa Maendeleo ya
Miaka Mitano.
Akizindua
mafunzo hayo yatakayofanyika kwa siku tani katika kanda ya kaskazini jiijjini
Arusha, Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango anayeshuhghulika na Biashara
za Kimataifa Bw. Paul Sangawe alibainisha kuwa lengo kuu la mafunzo haya
limejikita katika kuimarisha uwezo wa maafisa mipango ili waweze kuibua miradi
inayotekelezeka kwa urahisi na ufanisi.
Uwepo wa
mwongozo huu katika uwekezaji wa miradi ya umma utasaidia kuboresha usimamizi
na utekelezaji wa miradi ya umma kwa kuonyesha taratibu za kuzingatiwa ili
kuhakikisha miradi iliyochaguliwa inaendana na bajeti ya maendeloa ya taifa.
“Baada ya mafunzo haya, ni mategemeo yetu kuwa
mwongozo huu utawasaidia maafisa mipango kufanya upembuzi makini na uliyo
sahihi ili kuja na miradi bora itakayotuepusha na matumizi mabaya ya fedha za
umma saula ambalo kwa kipindi cha nyuma limekuwa likijitokeza huko nyuma. Hivyo
jitihada hizi ni vema zikazaa matunda chanya” alisema Bw. Sangawe.
Kutokana na
kutokuwepo kwa mwongozo wa kupembua na kuchagua miradi ya uwekezaji katika
sekta ya umma Tume ya Mipango imeandaa Mwongozo kwa maafisa mipango wote
nchini. Mwongozo huu utasadia kwa kuelekeza taratibu na kanuni zitakazotumika
kataka kuchagua, kufadhili, kutekeleza na hata kuperemba na kutathimini miradi
ya umma.
Ili kufikia
malengo ya kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, uchambuzi wa
kitaalamu katika masuala ya fedha, athari za kiuchumi na kijamii katika miradi tajwa inapaswa
kusimamiwa vema ili kuleta uwiano sawia kati ya miradi hiyo iliyochaguliwa na
bajeti ya taifa ya miradi ya maendeleo.
“Lengo hilo linabeba matarajio ya wananchi
wengi, japokuwa si suala ambalo ni rahisi kutekeleza bila kuwa na nidhamu
katika uchaguzi wa miradi. Namana pekee ya kulifikia hii ndoto ni kwa
kuhakikisha kidogo tulichonacho tunakitumia katika vipaumbele vya msingi vya
taifa na inatumika ipasavyo” aliongeza Bw. Sangawe.
No comments:
Post a Comment