Just in : Msafara wa Makamu wa Rais Wapata Ajali, Mtwara - Wazalendo 25 Blog

Breaking

Glory to Story.


Post Top Ad


9 Sep 2016

Just in : Msafara wa Makamu wa Rais Wapata Ajali, Mtwara

Msafara wa makamu wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzani Samia suluhu hassani ambao ulikuwa unaelekea wilayani tandahimba ukitokea ikulu ndogo ya rais mtwara umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya mtwara

Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi wanne wa makamu rais.

Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka mtwara kuelekea tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.

Post Top Ad