Waziri
Mkuu Mh.Kassim Majaliwa akiwasili katika uwanja wa mpira wa Miguu wa
Kaitaba mjini Bukoba mapema leo,kwa ajili ya kuwapa pole nyingi wakazi
wa mji huo na kwingineko na pia kushiriki sala ya pamoja ya kuwaaga na
kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu,waliokuwa wamekumbwa na
tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea
idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha.
Tetemeko
hilo kubwa la ardhi lenye mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea
jana Septemba 10, 2016 katika mikoa mitatu ya Kanda ya Ziwa kadhalika
nchi za Burundi na Uganda.Mikoa ya Kanda ya Ziwa iliyopata athari kwa
mujibu wa taarifa ni Mwanza, Mara na Kagera nchini na kuripotiwa kuua
zaidi ya watu 15 na wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa sambamba na kubomoa
majengo mbalimbali.
Pichani
kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimuelekeza jambo Mkuu wa Mkoa wa
Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salim Mustafa Kijuu ,kabla ya kuanza sala
ya pamoja ya kuwaaga na kutoa heshima za mwisho kwa miili ya
marehemu,waliokumbwa na tukio la tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana
jioni na kupelekea idadi ya zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito
kupoteza maisha.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameongoza maelfu ya wananchi wa Manispaa ya Bukoba mjini
kuaaga miili ya watu 16 waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea
jana (Jumamosi, 10 Septemba, 2016 mkoani Kagera.
Tetemeko
hilo lilitokea jana Alasiri limesababisha vifo vya watu 16 na wengine 253
kujeruhiwa. Pia limesababisha maelfu ya wananchi kukosa makazi baada ya nyumba
840 kuanguka na nyingine 1264 zikipata nyufa yakiwemo majengo 44 ya taasisi
mbalimbali za umma.
Kufuatia
tukio hilo Waziri Mkuu ambaye alimuwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Magufuli
amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kufanya tathmini ya
athari zilizotokana na maafa hayo.
“Poleni
sana tukio hili ni kubwa na halijawahi kutokea nchini. Haya yote ni mapenzi ya
Mwenyezi Mungu. Tuendelee kuwa na imani na watulivu Serikali ipo pamoja nanyi na haitawatupa
mkono,” amesema.
Waziri
Mkuu amesema Kamati ya Maafa ambayo ipo katika Ofisi ya Waziri ya Mkuu
itakwenda wilaya za Kyerwa, Karagwe na Bukoba mjini kwa ajili ya kufanya
tathmini na kubaini athari zilizosababishwa na tetemeko hilo na kuona namna ya
kuwasaidia waathirika.
Wakati huo huo Waziri Mkuu amewaagiza
viongozi wa mkoa huo kuchukua hatua za haraka kwa kuwatafutia eneo salama la
kulala wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyakato ambayo mabweni yake yote
yameathirika na tetemeko hilo na hayafai kutumika.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shule hiyo na kujionea namna mabweni
ya shule hiyo yalivyopata nyufa hali iliyosababisha wanafunzi kulala uwanjani.
Pia
Waziri Mkuu ameiagiza Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kuangalia kama
kuna tetemeko linguine linaweza kutokea nchini ili Serikali iweze kuchukua
tahadhari pamoja na kutoa elimu kwa umma namna ya kujikinga.
Naye
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu amesema kwa sasa
wanaendelea na jukumu la kuwatafutia makazi wananchi ambao nyumba zao zimeanguka.
Pia mkoa unaendelea kufanya tathmini ya kina kujua athari zilizosababishwa na
tetemeko hilo.
Awali
Waziri Mkuu alitembelea Hospitali ya Mkoa wa Kagera ambako majeruhi 170
wamelazwa na kutoa pole na kwamba anawaombea kwa Mwenyezi Mungu wapone haraka
na wenye matatizo ambayo yanahitaji matibabu kwenye hoispitali kubwa Serikali
itahakikisha wanapelekwa huko na kuhudumiwa.
IMETOLEWA
NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI,SEPTEMBA 11, 2016
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akimuelekeza jambo Mbunge wa jimbo la BUkoba
Mjini,Mh Wilfred Lwakatare,kabla ya kuanza sala ya pamoja ya kuwaaga na
kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu,waliokumbwa na tukio la
tetemeko la Ardhi ambalo limetokea jana jioni na kupelekea idadi ya
zaidi ya watu 15 akiwemo na mama mja mzito kupoteza maisha.
Baadhi ya ndugu na jamaa waliofika katika uwanja wa Kaitaba kushiriki sala ya pamoja ya kuwaaga wapendwa wao
Askofu
Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akisoma majina ya
masanduku yaliyobeba miili ya marehemu,tayari kwa kuagwa kwa pamoja
katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Askofu
Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akiwa na baadhi ya
viongozi wengine wa dini wakitazama majina ya masanduku yaliyobeba miili
ya marehemu,tayari kwa kuagwa kwa pamoja katika uwanja wa Kaitaba mjini
Bukoba mkoani Kagera.
Askofu
Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akiwa na baadhi ya
viongozi wengine wa dini wakiwa katika uwanja wa Kaitaba kushiriki sala
ya pamoja ya kuaga miili ya marehemu waliokumbwa na tetemeko la Ardhi
hapo jana mjini Bukoba mkoani Kagera.
Baadhi ya Masanduku yenye miili ya marehemu walioathiriwa na tetemeko la Ardhi hapo jana mjini Bukoba mkoani Kagera.
No comments:
Post a Comment