Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga ameuagiza uongozi wa Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS), na Wakala wa Majengo Nchini (TBA), mkoa wa Kagera kufanya
tathmini ya kina kwenye miundombinu ya barabara, madaraja na majengo ya
Serikali yalioathirika na tetemeko la ardhi.
Eng.
Nyamhanga ametoa agizo hilo Mkoani Kagera mara baada ya kukagua athari
za tetemeko la ardhi katika barabara za Bukoba- Mtukula, Kyaka-Bugene na
jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Tanzania na Uganda ambapo
amesema ni muhimu kufanya utafiti wa kitaalam katika miundombinu hiyo
kabla ya hatua za ukarabati kuanza.
Amesema kufanyika kwa utafiti huo utasaidia kubaini athari nyingine zilizojificha ambazo zimetokana na tetemeko hilo.
“Undeni
kikosi kazi cha wataalam maramoja waweze kuchunguza ili kujua sehemu
mbalimbali zilizoathirika ili tuweze kuzitengeneza mapema iwezekanvyo”,
amesema Eng. Nyamhanga.
Katika
hatua nyingine Eng. Nyamhanga amemuagiza Mkandarasi wa Kampuni ya M/S
China Henan International Cooperation Group Co. Ltd (CHICO) inayojenga
barabara ya Kyaka-Bugeni (KM 59.1) kumaliza kipande cha Kilomita mbili
katika barabara hiyo ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.
Amesema
kuwa kukamilika kwa kipande hicho kutaimarisha hali ya usafiri wa
wananchi katika wilaya za Bukoba na Karagwe na hivyo kuhuisha shughuli
za kiuchumi kwa wakazi wa Mkoa wa Kagera.
Eng.
Nyamhanga yupo mkoani Kagera kukagua athari za uharibifu wa miundombinu
kufuatia tetemeko la ardhi lililopiga mikoa ya Kagera, Mara na Mwanza
Septemba 10 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu takribani 17,
majeruhi zaidi ya 100, uharibifu wa nyumba takribani 800 na miundombinu.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto) akikagua sehemu ya barabara ya
Bukoba-Mtukula ambayo imepata athari kutokana na tetemeko la ardhi
lilitokea Mkoani Kagera hivi karibuni. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Kagera Eng. Andrea Kasamwa.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto), akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala
wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Kagera Eng. Andrea Kasamwa (kulia)
wakati alipokagua Daraja la Kyaka katika Mto Kagera.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga (wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa
kampuni ya M/S China Henan International Cooperation Group Co. Ltd
(CHICO) inayojenga barabara ya Kyaka-Bugeni (KM59.1), Mkoani Kagera.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga (kulia), akikagua daraja la Mwise lililopo katika
barabara ya Bukoba- Mtukula.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga (wa tatu kushoto), akikagua kipande cha Barabara
ya Kyaka-Bugeni (KM59.1 ) inayojengwa kwa kiwango cha lami, Mkoani
Kagera.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Afisa
Mfawidhi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Bw. Samweli Mori wakati alipokagua
jengo la Kituo cha Pamoja cha Forodha ambacho kimeathirika na tetemeko
la ardhi lililopo Mtukula Mkoani Kagera.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi),
Eng. Joseph Nyamhanga (wa pili kulia), akikagua jengo la Kituo cha
Pamoja cha Forodha ambacho kimeathirika na tetemeko la ardhi lililopo
Mtukula Mkoani Kagera.
Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment