Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka
mkandarasi M/S Hanil Jiangsu J/V anayejenga barabara ya Sakina-Tengeru
yenye urefu wa KM 14.1 na barabara ya mchepuo (Arusha bypass) yenye
urefu wa KM 42.4 kuhakikisha barabara hizo zinakamilika ifikapo mwezi
Machi na Oktoba mwakani.
Profesa Mbarawa amesema hayo mara baada ya kukagua ujenzi barabara hizo na kujiridhisha na hatua iliyofikiwa kwa barabara zote.
“Meneja
hakikisha ujenzi wa barabara hizi unakwenda sambamba na ujenzi wa
sehemu ya barabara inayoelekea Ikulu ya mjini Arusha ili kuiunganisha
vizuri barabara hiyo kwa kiwango cha lami”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akielekea
kukagua kingo za Daraja la Themi linalojengwa katika barabara ya
Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 jijini Arusha.
Amemtaka
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw. Gabriel Daqarro kushirikiana na Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS), mkoani humo kuhakikisha maji yanayopita
kwenye madaraja yaliyopanuliwa kufuatia ujenzi unaoendela hayasababishi
mafuriko kwenye makazi ya wananchi.
Kwa
upande wake Meneja wa TANROADS mkoa wa Arusha Eng. Johnny Kalupale
amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa ujenzi wa barabara mkoani
Arusha utakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa.
“Tumejipanga
kuhakikisha barabara ya Sakina-Tengeru na ile ya mchepuo zote
zitakamilika kama ilivyopangwa ili kupunguza msongamano hali
itakayovutia ongezeko la watalii na hivyo kukuza uchumi wa mkoa wa
Arusha”, amesema Eng. Kalupale.
Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua uwanja wa ndege wa
Arusha na kusisitiza kuwa nia ya Serikali ni kuupanua uwanja huo ambao
ni wa nne kwa uingizaji wa mapato nchini ili kuondoa msongamano uliopo
sasa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata
maelezo kutoka kwa Mhandisi Mkazi Shin Pil Soo wakati akikagua Daraja la
Nduruma lenye urefu wa mita 60 linalojengwa katika barabara ya
Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 jijini Arusha.
“Wakati
Serikali tunajipanga kuongeza uwanja huu na nyinyi mjipange kuongeza
mapato ili jitihada za Serikali ziendane na ubunifu wa watendaji”,
amesisitiza Prof. Mbarawa.
Naye
Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), mkoa wa Arusha Bw.
Elipid Tesha amesema uwanja huo ambao ni kitovu cha utalii katika
ukanda wa Kaskazini ukiongezwa utaruhusu ndege nyingi kutua na hivyo
kuuongezea mapato ambapo kwa sasa takribani miinuko 110 ya ndege
hufanyika kila siku katika uwanja huo.
“Kwa
sasa uwanja wa ndege wa Arusha una barabara ya kurukia yenye urefu wa
KM 1.6 hali inayosababisha baadhi ya ndege kushindwa kuutumia ila
mkakati wa uwanja huo ni kuuongeza uwe na urefu wa KM 2.5”, amesisitiza
Bw. Tesha.
Uwanja wa Ndege wa Arusha uliojengwa mwaka 1956 ikiwa ni mkakati wa
kuboresha huduma za utalii katika mkoa huo uko KM 7 kutoka Arusha Mjini
na una eneo la ekari 280 na uzio unaoimarisha usalama wakati wote.
Muonekano
wa juu wa Daraja la Nduruma lenye urefu wa mita 60 linalojengwa katika
barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 jijini Arusha.
Meneja
wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoa wa Arusha Eng. Johnny
Kalupale (katikati), akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), alipokagua ujenzi wa
barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 na barabara ya Arusha
mchepuo (bypass), yenye urefu wa KM 42.4 jijini Arusha.
Muonekano wa barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 ambayo upanuzi wake unaendelea jijini Arusha.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akishiriki
kikamilifu katika uwekaji wa kifusi cha tabaka la juu la zege kabla ya
kumwaga lami katika barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1
ambayo ujenzi wake unaendelea.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akisalimiana
na baadhi ya wananchi wakati alipokagua ujenzi wa barabara ya
Sakina-Tengeru yenye urefu wa KM 14.1 ambayo ujenzi wake unaendelea.
No comments:
Post a Comment