Matukio : Wafanyakazi wa Mathayo Suleiman Foundation Wachangia Damu Hospitali ya Muhimbili - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


26 Sept 2016

Matukio : Wafanyakazi wa Mathayo Suleiman Foundation Wachangia Damu Hospitali ya Muhimbili



WAFANYAKAZI wa Mathayo Suleiman Foundation wachangia Dam katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. Mathayo Suleiman Foundation ni foundation inayojihusisha na kutoa huduma kwa maendeleo ya jamii na kuwaunganisha wanawake pamoja na vijana katika shughuli za uzalishaji mali.

Pia na Foundation Inayosaidia vikundi vyenye shida na mahitaji maalumu kama watoto yatima.

Mwenyekiti Mtendaji wa Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaphy Mathayo akizungumza na wafanyakazi hao amesema kuwa leongo kuu la kuchangia damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni kuokoa maisha ya wahitaji wa damu wanaofikishwa katika hospitali hiyo.

 Mwenyekiti Mtendaji wa Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaphy Mathayo akizungumza kabla ya kuingia kuchangia Damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Amesema kuwa lengo la kuchangia damu katika Hospitali ya Taifa ni kuokoa maisha ya watu wenye mahitaji ya kuongezewa damu.
 Mratibu wa Mathayo Suleiman Foundation, Banga Suleiman akizungumza na wafanyakazi wa Foundation hiyo pamoja na kuwashukuru Wafanyakazi wa Mathayo Suleiman Foundation jinsi walivyojitoa katika kusaidia na kuokoa maisha ya watu wenye mahitaji ya kuongezewa damu katika hospitali ya Mhimbili jijini Dar es Salaam leo. 
Afisa Ustawi wa jamii na Mama ushauri nasihi katika huspitali ya Taifa ya Muhimbi kitengo cha Kuchangia Damu, Mama Makishi akizungumza na wafanyakazi wa Mathayo Suleiman Foundation kabla ya kuingia katika chumba cha kuchangia Damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo, amewaeleza fyakula vya kula kabla na baada ya kuchangia damu pamoja na maradhi ya kupima pamoja na wingi wa Damu.

Pia amewaomba wafanyakazi hao walioweza kuchangia damu wawe wanachama kwani kwa kila mwanachama anatakiwa kuchangia zamu kwa mwaka mara mbili pia faida ya kuwa mwanachama atakapo kuwa na mahitaji ya damu atapewa kutoka enki ya damu. 
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mathayo Suleiman Foundation  wakisubiri kwenda kupima baadhi ya maradhi ndio waingie katika chumba cha kutolea damu.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaphy Mathayo  akijiandaa kwenda kuchangia damu.
  Mwenyekiti Mtendaji wa Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaphy Mathayo  akiandaliwa kwaajili ya kuchangia damu.
 Mwenyekiti Mtendaji wa Mathayo Suleiman Foundation, Eliasaphy Mathayo  akizungumza na mtoa huduma wakati akiendelea kuchangia damu.




  




   

 Baadhi ya ya wafanyakazi wa Mathayo Suleiman Foundation wakichangia damu katika chumba cha kuchangia damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Mathayo Suleiman Foundation wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuchangia damu.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mathayo Suleiman Foundation wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuchangia damu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.




Baadhi ya wafanyakazi wa   Mathayo Suleiman Foundation wakisubiri kuingi kuchangia damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad