Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,aiagiza
Mamlaka ya uthibiti wa usafari wa majini na nchi kavu (SUMATRA) kuendelea kutoa
leseni za magari aina ya Noha kwa Mkoa
wa Arusha,hasa kwa yale yanayofanya safari zake kati ya Arusha mjini kuelekea
Karatu na Longido.
Aigizo
hilo amelitoa baada yakupata malalamiko kutoka kwa uwongozi wa wamiliki
wa magari hayo ukiongozwa na wenyekiti wake Bwana Ally Mkali alisema
SUMATRA wamesitisha utoaji wa leseni za
kawaida kwa magari ya Noha na wataanza kutoa leseni kwa yale yatakayokuwa tayari kutembea umbali
wa Kilometa 50 tu.
“Nawaagiza SUMATRA kuendelea kutoa leseni kwa
utaratibu uliopo kwasasa na wakati huo mjipange kukutana na wadau wote
nakujadili namna yakulitatua swala la magari haya kutembea umbali wa Kilometa 50 hasa kwakuangalia mazingira ya Mkoa wa Arusha
nimagumu na kwakulitekeleza hilo
litaongeza gharama kwa wananchi”,alisema Gambo.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo kwa Mkoa wa Arusha
Bwana Allen Mwanri, alisema sababu zilizopeleka SUMATRA kupitisha utaratibu huo
kwa magari hayo ni kutoweza kumudu kutembea umbali mrefu kwani ni
hasara napia inahatarisha maisha ya abiria.
“Tuliamua kupendekeza utaratibu huu kwasababu
magari mengi ya Noha yalionyesha kushindwa kutembea umbali mrefu na huku yakibeba abiria zaidi yakiwango
kinachoitajika cha watu nane”,alisema Mwanri.
Aidha Mkuu wa kikosi cha usalama barabara Mkoa
kamanda Nuru Selemani,amewataka madereva wa magari hayo aina ya Noha kufuata
sheria na taratibu za barabarani ilikulinda usalama wao na abiria,na kwakushindwa
kufanya hivyo basi sheria zitachukuliwa dhidi yao.
Maamuzi hayo yalitolewa baada ya Mkuu wa Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kuwatembelea
madereva wa magari hayo maeneo ya standi
kuu ya Mkoa nakujionea hali halisi ya utoaji huduma kwa magari hayo
kwani mengi yalikuwa yamesitisha huduma hiyo kwakukosa leseni za usafirishaji.
|
No comments:
Post a Comment