Kikundi
cha Makerubi kutoka Manyara ambao walijiandikisha wakitokea Temeke
waliweza kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali katika shindano la
Gospel Star Search 2016 kwa kuweza kuimba kwa ustadi mkubwa. Shindano la
Nusu fainali lilifanyika katika viwanja vya Biafra - Kindononi jijini
Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Umati
wa watu waliohudhuria shindano la Gospel Star Search lililofanyika
mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra - Kinondoni jijini
Dar es Salaam.
Mshiriki
namba 4. Grace Madole akiimba katika jukwaa la Gospel Star Search
lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya Biafra -
Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu hakuweza kupenya hatua ya
fainali.
Mshiriki
namba 5. Winnypraise William akiimba katika jukwaa la Gospel Star
Search lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika viwanja vya
Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam. Mshiriki huyu alipenya kuingia
hatua ya fainali.
Shindano
la Gospel Star Search lilikuwa ni vuta nikuvute pamoja na mshiriki
namba 6. Willansia Lema kuimba kwa hisia ila hakuweza kufanikiwa kuingia
hatua ya nusu fainali ambayo iliweza kuingiza washiriki wapatao 10 na
kufanya washirikiki watano (5) kuaga mashindano.
Mshiriki namba 10. Flora Kachema alifanikiwa kuingia fainali.
Majaji
wa shindano la Gospel Star Search (GSS) kutoka kulia ni Mchungaji Sam
Mwangati, Sarah Ndossi na Fred Msungu wakiwa wamenyanyuka kuonyesha
heshima ya pekee kwa mshiriki ambaye aliweza kuvuta hisia zao.
Mshiriki Mdogo kuliko wote akiwa aliwavuta hisia majaji wakajikuta wanatoa heshima ya pekee kwa kusimama.
Wageni waliohudhuria shindano hilo wakifurahia kwa shangwe.
Nderemo na vifijo vilitawala.
Mshiriki huyo akiwa amewateka na kujikuta wakiimba kwa hisia wageni waliohudhuria.
Mshiriki
Sunday Lunkombe alifanya vyema kuliko wenzake na kufanikiwa kuongoza
hakua ya kuingia fainali kwa kujizolea alama nyingi.
Washiriki wakionyesha umahili wa kuimba pamoja kabla ya kutangazwa kumi bora.
Meneja
Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali akionyesha vijana
walifanikiwa kuingia hatua ya fainali (kumi Bora) mara baada ya mchuano
mkali.
Kiongozi
wa Majaji, Mchungaji Sam Mwangati akisoma majina ya vijana walifanikiwa
kuingia hatua ya fainali ya shindano la Gospel Star Search 2016
lililofanyika katika uwanja wa Biafra - Kinondoni jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki iliyopita. Fainali za shindano hili zinatarajiwa
kufanyika jumapili ya Septemba 18, 2016 katika ukumbu wa Milado, Sinza
jijini Dar es Salam.
Na Cathbert Kajuna wa Kajunason blog.
Vijana
10 wamefanikiwa kuingia hatua ya fainali katika shindano la kumtafuta
mkali wa kuimba nyimbo za injili 'Gospel Star Search 2016' lililofanyika
katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.
Akizungumza Meneja Mradi wa Gospel Star Search 2016, Samwel Sasali
alisema kuwa ni vyema vijana wakazingatia mafundisho yote waliyopatiwa
na walimu wao ili waweze kushindana kwa uweledi na ustadi wa hali ya
juu.
Alisema
wakati umefika wa vijana kutambua talanta au vipaji walivyopewa na
mwenyezi Mungu ili viwaletee manufaa katika kumtangaza Bwana Yesu
Kristo.
"Tokea tumeanza kuzunguka kukusanya vijana hakika tumeweza kupata vijana
wengi wenye vipaji na kuonyesha kuwa mwamko wa vijana katika kutambua
vipaji vyao umekuwa mkubwa, hakikuwa jambo jepesi sana ila yote kwa yote
tunamshukuru Mwenyezi Mungu aliyeweza kufanikisha yote", alisema
Sasali.
Aliongeza
kuwa shindano la Gospel Star Search 2016 liliweza kupata washiriki
wengi ila wakafanyiwa mchujo na kupatikana wapatao 15 ambao waliweza
kuingia hatua ya nusu fainali na wakafanya mchuzo katika viwanja vya
Biafra wakapatikana 10 ambao wameingia katika kikaango na ipatapo
Septemba 18, 2016 Jumapili katika ukumbi wa Milado, Sinza ndipo fainali
zitakapofanyika.
Vijana 15 waliokuwa wameingia nusu fainali ni 1. Makerubi, 2. Enighenja
Mmbaga, 3. Upendo John, 4. Grace Madole, 5. Winnypraise William, 6.
Willansia Lema, 7. Rogate Kalengo, 8. Suleiman Wilson, 9. Innocent
Eliya. Wengine ni 10. Flora Kachema, 11. Steve Njama, 12. Winnifrida
Dudu, 13. Calvin John, 14. Sunday Lunkombe na 15. Beda Andrew.
Waliofanikiwa kuingia Fainali ni vijana 10 ambao ni 1. Makerubi, 2. Beda
Andrew, 3. Winnypraise William, 4. Rogate Kalengo, 5. Suleiman Wilson,
6. Flora Kachema. Wengine ni 7. Steve Njama, 8. Winnifrida Dudu, 9.
Calvin John na 10. Sunday Lunkombe.
Shindano la GSS limedhaminiwa na Maendeleo Bank, Grace Product, Brand
exponetial, Kiango media, Clouds Media Group, Fm studios (Faith music
lab) na 3D.
No comments:
Post a Comment