Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa
maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho
kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu
Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete
akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune
Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa
habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya
kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi.
Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum
kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea
Septemba mosi .
Eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum
kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea
Septemba mosi .
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Mbarali,Mbeya .
SHIRIKA
la Hifadhi
za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio la kupatwa kwa jua
linalotarajia kuonekana Septemba mosi mwaka huu kufungua lango la Ikoga
katika
wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI
ya Taifa ya Ruaha
Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya
kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction
ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
Pascal Shelutete anasema kuongezeka kwa
geti la Ikoga ni fursa kubwa ya
kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa eneo la Ihefu
linakivutio kikubwa cha wanyama
wa aina mbalimbali .
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema
Wilaya hiyo ina vivutio vingi, hivyo
amewataka wananchi watakaofika kuangalia
kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio
vilivyopo Wilayani humo.
Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi
majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga
Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya .
No comments:
Post a Comment