Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akikata keki
kuashiria uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo kwenye duka
la huduma kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni
hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba pamoja na Mkuu wa
Kitengo cha Biashara TTCL Kanda ya Dar es Salaam, Bi. Jane Mwakalebela
(kulia) wakishuhudia tukio hilo.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri
Waziri Kindamba (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
(kushoto) wakigonganisha glasi za mvinyo mara baada ya mkuu huyo wa mkoa
kuzinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo kwenye duka la huduma
kwa wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini
Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki Kaimu Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba
kwenye uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki Afisa Mkuu
wa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Bw. Peter Ngota kwenye uzinduzi wa
Wiki ya Huduma kwa Wateja wa TTCL leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimlisha keki mmoja wa
wateja wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa
Wateja wa TTCL leo.
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amezitaka taasisi na mashirika
ya umma yaliopo chini ya mkoa wake kuiunga mkono Kampuni ya Simu ya
kizalendo Tanzania (TTCL) kwa kuanza kuzitumia bidhaa za kampuni hiyo
hasa kwenye shughuli za mawasiliano ili kuonesha uzalendo kwa vitendo.
Makonda
ametoa kauli hiyo leo Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam
alipokuwa akizinduwa Wiki ya Huduma kwa Wateja wa kampuni ya TTCL, huku
akiahidi kuzishawishi taasisi na mashirika ya umma yanayofanya kazi
chini ya utawala wake kuhakikisha wanatumia huduma za TTCL ili kuiunga
mkono kampuni hiyo ya kizalendo ya mawasiliano.
Alisema
Serikali imeonesha nia njema ya kuirejesha TTCL katika hali nzuri baada
ya kuirejesha kwa asilimia 100 chini ya umiliki wake, hivyo kuyataka
mashirika na taasisi za umma kuunga mkono juhudi za Rais wa Tanzania,
Dk. John Pombe Magufuli kuirejesha kampuni hiyo chini ya umiliki wa
serikali kwa asilimia 100.
Alisema
yete kama kiongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam atahakikisha ofisi zote za
umma zilizopo chini ya mkoa wake zitatumia huduma za TTCL na endapo
watendaji wa TTCL sinazosita kutumia watoe taarifa ili yeye ahoji ni
kwanini wanapinga agizo hilo.
Aidha
Mkuu wa Mkoa huyo alisitaka baadhi ya taasisi za umma wadaiwa sugu wa
TTCL walipe madeni yao mara moja na zile zinazokaidi zifikizwe kwenye
mkono wa sheria (mahakamani) kwa ajiri ya taratibu za kisheria. Alisema
kampuni itafanya vizuri kihuduma endapo wateja wanaopewa huduma wanalipa
kwa wakati ili iweze kuboresha huduma zake kwa wateja wote.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na mwenyeji
wake huku akionesha alama ya mabadiliko inayotumiwa na TTCL.
Kwa
upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba
akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa Makonda alisema Kampuni
ya Simu Tanzani iliianza mchakato wa kuleta mabadiliko ndani ya kampuni
hiyo tangu mwaka 2014, mpango uliopewa jina la 'TTCL Business
Transformation Project' ambao ulilenga kuongeza tija na ufanisi katika
uzalishaji na uwajibikaji ili kutoa huduma bora kwa Wananchi na Wateja
wetu wote wa ndani na nje ya Tanzania.
Aliyataja
miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi chote cha mabadiliko
ya kibiashara ni pamoja na kuirejesha Kampuni ya TTCL kumilikiwa na
Serikali kwa asilimia 100 baada ya kuondoka kwa aliekuwa mbia mwenza,
kupatikana kwa Masafa yanayowezesha kutolewa kwa huduma za 3G/4G na
utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kuboresha huduma. Kindamba
aliongeza mafanikio mengine ni kupatikana kwa fedha kutoka kwenye vyanzo
mbalimbali ikiwemo Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB), Kupatikana fedha
kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambazo zinatumika kwa ajili
ya kupeleka mawasiliano vijijini na Ujenzi na ukarabati wa miundombinu
ya mtandao wa Mawasiliano, mitambo chakavu, kusimika mitambo ya GSM-2G,
UMTS- 3G na LTE- 4G. "...pia katika eneo la Biashara; Tumeendelea na
juhudi za kutangaza na kuitambulisha huduma ya 3G/4G katika jiji la Dar
es salaam, bidhaa nzuri ambazo zinakidhi mahitaji ya wateja zimekuwa
chachu ya wananchi kuanza kuvutiwa na bidhaa za TTCL.
TTCL
tunatoa huduma ya T-TV ambayo wateja wanapata fursa ya kutazama
matangazo ya vituo mbalimbali vya Luninga kupitia simu zao za Smartphone
na tablet.
Pia,
TTCL imefanikiwa kuunganisha Hospitali Kuu za Mkoa wa Dar es salaam
katika Mkongo wa TTCL, hivyo kutengeneza mazingira mazuri kwa taasisi
hizo kuendesha huduma za afya kwa kutumia teknolojia yaani Afya-Mtandao
(E-Health)," alisema Kindamba.
Aidha
alisema wiki ya Huduma kwa Wateja, TTCL inalenga kutambua na kuthamini
mchango wa wateja, ambao wamekuwa chachu ya ukuaji wa Kampuni, huku
kampuni ikijipanga kuwatembelea wateja wake, kuzungumza nao na kuomba
ushauri wao ili tuweze kutoa huduma bora na endelevu ambazo zitaongeza
tija katika kazi zao.
"...Tumejipanga
vyema kufanya kazi kwa ufanisi, tunatekeleza kwa vitendo falsafa ya
Serikali yetu ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu. Tutatumia rasilimali
zetu vizuri ili Kampuni itoe mchango stahiki mageuzi yanayoendelea ya
kuifanya nchi yetu kupiga hatua kuelekea kuwa nchi ya Uchumi wa Kati,
Nchi ya Uchumi wa Viwanda.
Katika
kufikia lengo hili, huduma za Mawasiliano ni muhimu sana, na napenda
kukuhakikishia kwamba, kwa kutumia huduma za TTCL, lengo hili
litafikiwa," Alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (wa pili kulia) akimpa tuzo
mmoja wa wafanyakazi bora wa kampuni hiyo kwenye duka la huduma kwa
wateja na bidhaa za TTCL lililopo Makao Makuu ya kampuni hiyo jijini Dar
es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na
wafanyakazi bora wa TTCL waliozawadiwa kwenye uzinduzi wa wiki ya huduma
kwa wateja.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipiga picha na baadhi ya
viongozi waandamizi wa TTCL kwenye uzinduzi wa wiki ya huduma kwa
wateja. Meneja Uhusiano wa TTCL, Nicodemus Mushi akitoa ratiba fupi ya hafla hiyo kabla ya uzinduzi.
No comments:
Post a Comment