Rais Jacob Zuma amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa kiongozi wa chama tawala nchini humo cha African National Congress ANC.
Zuma alipata idadi kubwa ya kura zilizopigwa na wajumbe elfu nne wa chama hicho wakati wa mkutano wao uliofanyika Mangaung.
Tangu
mwanza wa zoezi hilo, Rais Zuma, alitarajiwa kushinda na idadi kubwa ya
kura dhidi ya mpinzani wake wa pekee ambaye pia ni naibu makamu wa rais
Kgalema Motlanthe.
Bwana Motlanthe sasa amepoteza nafasi yake ya
naibu kiongozi wa chama hicho na mahala pake pamechukuliwa na
mfanyabiashara maarufu na mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi Cyril
Ramaphosa, ambaye sasa atakuwa makamu wa rais wa Afrika Kusini.
Ramaphosa makamu mpya wa rais
Mshindi wa nafasi hiyo ndiye atakayekuwa na nafasi ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2014.
Chama cha ANC kimeshika hatamu nchini Africa Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.
Polisi nchini humo, hapo jana waliwatia mbaroni
watu wanne baada ya taarifa kuzagaa kwamba walikuwa na mpango wa
kulipuwa ukumbi unaotumiwa na wajumbe hao wa chama cha ANC.
Baada ya uchaguzi huo kucheleweshwa kwa masaa
kadhaa, zoezi la kupiga kura lilianza saa sita usiku na kukamilika
majira ya saa moja asubuhi kwa saa za Afrika Kusini.
Wajumbe hao walioonekana wamechoka huku wakijifunika mablanketi walionyesha vidole vyao vikiwa na alama ya wino.
Wajumbe hao wamekuwa wakipiga kura kwa ajili ya nafasi ya uongozi wa juu wa chama hicho.
Wafuasi wa rais Zuma, tayari wanaendelea kusheherekea, kufuatia ushindi huo mkubwa.
Rais Zuma analaumiwa kwa kushindwa kupunguza
umaskini au kutatua tatizo la ufisadi ndani ya chama cha ANC na
serikali, wakati mwezi wa nane mwaka huu watu walishangazwa na jinsi
polisi walivyowapiga risasi na kuwauwa wachimba madini 34 ambao walikuwa
wamegoma. Na BBC Swahili.com
No comments:
Post a Comment