Pamoja
na kuwa bora utoaji wa huduma za kibenki lakini pia benki ya NMB
imejipanga kuhakikisha inakuwa pia bora katika kusaidia jamii na katika
kudhihilisha hilo imetoa msaada wa vifaa vya kutumia darasani na vya
michezo kwa watoto walio na usonji (autism) ambao wanasoma katika shule
ya msingi Mbuyuni, iliyopo Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam.
Akielezea
kuhusu msaada huo, Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky
Bishubo alisema wameamua kutoa msaada kwa shule hiyo kwa ajili ya
kuwasaidia watoto wenye usonji kusoma katika mazingira mazuri hasa
kutokana na hali zao jinsi zilivyo.
Meneja
wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo akizungumza wakati
wa kukabidhi vifaa vya shuleni kwa wanafunzi wa usonji katika shule ya
Msingi Mbuyuni.
"NMB
kila mwaka tunatenga asilimia moja ya faida ambayo tunaipata katika
kusaidia jamii, tumeshatoa misaada mingi kama madawati na sasa tuliona
tuwasaidie watoto hawa na tunaamini msaada wetu utaweza kuwasaidia kwa
kiasi kikubwa," alisema Bi. Bishubo.
Kwa
upande wa mgeni rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa
Ustawi wa Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi aliwashukuru
NMB kwa msaada ambao wamewapatia shule ya Mbuyuni na kuwataka kuendelea
kuwa na moyo huo kwa kutoa msaada katika shule zingine zilizo na
mahitaji.
Mgeni
rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akiwashukuru NMB kwa msaada
ambao wamewapatia ambao unakadiriwa kuzidi Milioni 7.
Alisema
licha ya serikali kufanya jitihada mbalimbali lakini bado inahitaji
wadau wengine wa kusaidiana na kama kunakuwa na wadau kama NMB ambao
wanajitoa kusaidia jamii basi wanakuwa wadau wa ukweli ambao wanaunga
mkono juhudi za serikali kuleta maendeleo.
"Kwa
nia yenu ya kusaidia jamii basi nyie mnaipatia kabisa serikali sababu
inajitahidi kuleta elimu bora na hata kwa watoto hawa ambao bado kuna
changamoto ya vifaa kwahiyo sisi tuwashukuru kwa msaada wenu na msisite
tena kutusaidia siku tukiwafata kwa kuomba msaada," alisema Mushi.
Na Rabi Hume, MO BLOG
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Mbuyuni, Dorothy Malecela akitoa neno la
shukrani kwani niaba ya uongozi wa shule na wanafunzi. (Picha zote na
Rabi Hume - MO BLOG)
Mgeni
rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akimshukuru Meneja wa Kanda
ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo kwa msaada ambao wamewapatia.
Mgeni
rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi na Meneja wa Kanda ya Dar es
Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo wakicheza na wanafunzi wa Shule ya
Msingi Mbuyuni.
Mgeni
rasmi katika makabidhiano ya msaada huo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii
kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Rabikira Mushi akipokea vifaa vya michezo
kutoka kwa Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa NMB, Bi. Vicky Bishubo
ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Mbuyuni.
Mwonekano wa baadhi ya vifaa vya michezo ambavyo NMB imetoa msaada kwa Shule ya Msingi Mbuyuni.
No comments:
Post a Comment