Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa
Serikali haitaendelea na ujenzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa
Songwe uliopo mkoani Mbeya mpaka tume ya watalamu iliyoundwa kuchunguza ili
kujiridhisha kama utaratibu ulizingatiwa kabla ya kuaza ujenzi huo.
Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua jengo hilo linalojengwa na
mkandarasi wa Kampuni ya Db Shapriya ya Tanzania ambapo amesema hadhi ya
jengo hilo hairidhishi hivyo ipo haja ya kujiridhisha kama taratibu zote zilifuatwa kabla ya
ujenzi.
Amebainisha kazi ya tume hiyo ya wataalamu ni kuhakiki namna utaratibu wa kumpata
mkandarasi ulivyofanywa, gharama halisi za mradi na fedha iliyolipwa kwa mkandarasi
kama inaendana na thamani ya jengo hilo.
"Serikali haiwezi kutoa fedha ya kumalizia jengo hili kabla ya kujiridhisha ili kuhakikisha
fedha tutakazozitoa zitatumika kulingana na ilivyopangwa na thamani ya fedha
inaendana na jengo lenyewe", amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha Waziri Prof. Mbarawa ameeleza ili kuwa na miundombinu imara na ya kudumu ni
lazima kuhakikisha miradi ya ujenzi wa miundombinu inasimamiwa vizuri na taratibu
za kupata mkandarasi bora zinafuatwa.
"Kutokuwa na miundombinu isiyo imara ni sababu ya wahusika kuweka mbele maslahi
binafsi na siyo ya Taifa", amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa
Pia ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha
makosa yaliyojitokezo kwenye ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa
Mwanza hayajirudii katika kiwanja hiki.
Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songwe Bw. Hamisi Amiri
amemhakikishia Waziri Mbarawa kusimamia ujenzi uliobaki kwa kuzingatia taratibu na
makubaliano yaliyowekwa ili jengo hilo lidumu kwa manufaa ya Taifa na Mkoa.
Uwanja wa Songwe ni kiungo muhimu kwa wananchi wa mikoa ya Katavi, Rukwa,
Njombe na Ruvuma na katika mwaka huu wa fedha umetengewa kiasi cha shilingi
bilioni 10 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la abiria na taa uwanjani hapo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipata maelezo
ya mfumo wa utabiri wa hali ya hewa katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe (SIA) kutoka kwa
Mtaalam wa masuala ya hali ya hewa uwanjani hapo, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani
Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipata maelezo
kutoka kwa Bw. Baraka Mwambipile kuhusu namna ndege zinavyoongozwa wakati wa kuruka
na kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani
Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata ufafanuzi wa
michoro ya ujenzi wa jengo la abiria kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
(TAA) wakati alipokagua Uwanja wa Ndege wa Songwe, Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa
Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) kuhusu ujenzi wa jengo la pili la abiria
katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, wakati alipokagua uwanja huo Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia)
akiendelea na ukaguzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Songwe, Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi
wa wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe , Mkoani Mbeya.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia) akitoa maelekezo
kwa Mkandarasi wa kampuni ya Shapriya Co Ltd anayejenga jengo la pili la abiria wakati
alipokagua uwanja wa kimataifa wa Songwe, Mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment