Mkandarasi
Jianx-Geo Engineering Group Corporation kutoka China anayejenga sehemu
ya barabara ya Sumbawanga Mjini-Chala-Kanazi kwa kiwango cha lami
amepewa wiki mbili kurejesha vifaa vya ujenzi katika eneo la kazi ili
kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo ambao umeonekana kusuasua
kutokana na ukosefu wa vifaa vya kutosha.
Kauli
hiyo imetolewa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa, wakati alipokagua mradi wa ujenzi wa barabara ya
Sumbawanga-Namanyere-Mpanda Mkoani Rukwa.
Waziri
Prof. Mbarawa amesema barabara hiyo imegawanywa katika sehemu mbili
ambazo ni Sumbawanga Mjini-Chala-Kanazi KM 75 na Kanazi-Kizi-Kibaoni KM
76.6 ili kuhakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na viwango
kulingana na mkataba.
“Hakikisheni
baada ya wiki mbili vifaa vinakuwepo katika eneo la kazi na mnatekeleza
wajibu wenu kukamilisha barabara hii kwa wakati tuliokubaliana ili
ianze kutumiwa na wananchi”, amesema Prof. Mbarawa.
Waziri
Prof. Mbarawa ameongeza kuwa wananchi wanamatarajio makubwa na barabara
hiyo kwa muda mrefu hivyo Mkandarasi ahakikishe kazi ya ujenzi katika
kipande kilichobaki kwa kiwango cha lami inamalizika ifikapo mwezi Julai
mwakani ili kuharakisha shughuli za kimaendeleo mkoani hapo.
Aidha,
amemtaka mkandarasi huyo kukamilisha mzani wa kupima uzito wa magari
katika kijiji cha Kanondo KM 5 kutoka Sumbawanga mjini ifikapo mwezi
Agosti mwaka huu kwa lengo la kudhibiti uzito wa magari yanayofanya
shughuli za kusafirisha mizigo na abiria katika barabara hiyo.
Kwa
upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa
Rukwa, Eng. Masuka Mkina amemuhakikishia Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa
barabara zote utazingatia viwango na utakamilika kwa wakati.
"Nikuhakikishie
kuwa tutasimamia na kuzingatia viwango vilivyowekwa katika mradi wa
ujenzi huu ili wananchi wanufaike na kuongeza uchumi wa mkoa ",amesema
Eng. Mhina.
Ujenzi
wa barabara ya Sumbawanga-Namanyere-Mpanda kwa kiwango cha lami
unagharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa jumla ya kiasi cha Shilingi
bilioni 150.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Mkandarasi anayejenga barabara ya Sumbawanga Mjini-Chala-
Kanazi yenye urefu wa KM 75 alipokagua ujenzi wa barabara hiyo.
Mkandarasi
anayejenga barabara ya Kanazi-Kizi-Kibaoni yenye urefu wa KM 76.6
akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa wakati alipokagua ujenzi huo. Katikati ni Meneja wa
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Rukwa Eng. Masuka Mkina.
Mbunge
wa Jimbo la Nkasi kaskazini Mhe. Ally Kessy (mwenye kofia) akieleza
jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa wakati alipokagua miundombinu ya Bandari ya Kipili, Mkoa wa
Rukwa.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Kulia)
akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw. Sandali
Kaisi (kushoto) kuhusu uboreshwaji wa kiwanja hicho wakati alipotembelea
kiwanja hicho.
Meneja
wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw. Sandali Kaisi (wa kwanza kushoto)
akitoa maelezo ya hali ya miundombinu kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia kwake) wakati Waziri
alipokagua kiwanja hicho.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili
Kulia) akitoa maelekezo kwa Meneja wa kiwanja cha ndege cha Rukwa Bw.
Sandali Kaisi (wa kwanza kushoto) wakati alipokagua kiwanja hicho.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa
maelekezo kwa Afisa Uendeshaji wa Bandari ya Kipili Bw. Hamis Msellem
wakati alipokagua miundombinu ya bandari hiyo wilaya ya Nkasi, Mkoani
Rukwa. Kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo la Nkasi kaskazini Mhe. Ally
Kessy.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua
jambo kwa Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini Mhe. Ally Kessy wakati
alipokagua miundombinu ya bandari hiyo, Mkoani Rukwa.
Mbunge
wa Jimbo la Nkasi kaskazini Mhe. Ally Kessy akiteta jambo na Waziri wa
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati
alipotembelea Jimboni kwake.
No comments:
Post a Comment