Na Bashir Yakub.
Unao
watoto wa namna mbalimbali. Unao uliowazaa ndani ya ndoa na
wale uliowazaa nje ya ndoa. Unawapenda sana wote kwa usawa
kwasababu wote ni watoto wako. Kuna suala la kifo na ungependa
baada ya kifo chako watoto wako wote wafaidi kidogo
ulichochuma. Lakini je hilo umelijengea mazingira.
Ni
muhimu sana ujue kuwa suala la watoto wako kufaidi ulichonacho
halitokani na matakwa yako, laa hasha bali linatokana na matakwa
ya sheria. Wewe waweza kuamua watoto wako wote wa nje ya ndoa
na wale wa ndani ya ndoa wapate mali lakini baadhi wakakosa
kutokana na msimamo wa sheria.
Ni
hapo unapotakiwa kuandaa mazingira yanayoendana na matakwa ya
sheria ili watoto wako wote waweze kufaidi machumo yako.
1.FANYA HAYA ILI KUWAWEZESHA WATOTO WA NJE YA NDOA KURITHI.
a. KWA WAISLAMU.
Kama
wewe ni muislam na una mtoto/watoto nje ya ndoa hakikisha
unaandika wosia ambao utampatia mali hata huyo mtoto wa nje
ya ndoa. Lakini lazima ujue kuwa mali yako yote uliyonayo ni
3/3 = (100%). Hivyo 2/3 ya mali yote ni lazima iende kwa
warithi halali ambamo mtoto wa nje ya ndoa hataingia kabisa.
Katika mali hiyo ya 2/3 wala haihitaji wosia kwakuwa tayari
sheria ya kiislam imeeleza vipi hiyo mali igawanywe.
Uhuru
wako wa kugawa mali kwa wosia upo katika 1/3 basi na si
vinginevyo. Na ni kusema kuwa mtoto/watoto wa nje ya ndoa haki
yao ipo katika 1/3 tu. Ikiwa utampatia mali zaidi ya 1/3 basi
anaweza kunyanganywa . Kwahiyo uelewe kuwa wosia utakaoandika
unahusu 1/3 ya mali tu.
Zingatia
kuwa usipoandika wosia kugawa 1/3 yote au sehemu yake kwa
mtoto/watoto uliowazaa nje ya ndoa basi hawatapata mali kabisa
baada ya kifo chako. Na hii ni kwasababu watoto hao
hawaruhusiwi kurithi kisheria. Kwahiyo utaona kuwa unachotakiwa
kufanya ili hao watoto wasikose ni kupiga hesabu ili kupata
1/3 ya mali yako na kuwapa yote au sehemu yake.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
No comments:
Post a Comment