Na Is-haka Omar, Zanzibar.
CHAMA
cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimewataka wananchi wanaoishi katika
maeneo yanayomilikiwa na chama hicho kuhakikisha wanafunga mikataba
rasmi ili kuepuka usumbufu wakati maeneo hayo yatakapohitajika kwa ajili
ya shughuli za kichama.
Kimesema
kuna baadhi ya wananchi waliopewa maeneo ya kuishi kwa muda kwa nia ya
kuwasaidia na badala yake wameyageuza kuwa makaazi yao ya kudumu jambo
ambalo sio sahihi.Akizungumza
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndg. Vuai Ali Vuai kwa nyakati
tofauti katika mwendelezo wa ziara ya kuhakiki mali na maeneo mbali
mbali yanayomilikiwa na CCM huko Mbweni Mkoa wa Magharibi Kichama.
Alisema
chama kinaendelea na zoezi la kuhakiki mali zake kutokana na kuongezeka
kwa vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watu wasiokuwa
waaminifu wanaotengeneza hati na mikataba bandia ya kujimilikisha mali
za chama hicho kinyume na utaratibu.
Ndg.
Vuai alifafanua kwamba katika hatua za kupunguza kero hizo chama
kimeamua watu wote ambao wamepewa kibinadamu sehemu za kuishi ama
kufanya biashara kwa muda katika maeneo yanayomilikiwa na CCM wafunge
mikataba rasmi ili chama kiweze kunufaika na rasilimali zake.
“
Watu waliopewa kwa dharura sehemu za kuishi na kufanya biashara kama
hatujawapa mikataba rasmi inayotambulikana kisheria, ambayo ni kielelezo
cha kumtambulisha nani mmiliki halali wa maeneo hayo baadae inaweza
kuwa fursa ya kufanya utapele na kusababisha usumbufu na lawama kwa
chama.
Tujaalie
kwamba mtu anaishi katika kiwanja cha Chama bila mkataba wa kisheria na
imetokea ameondoka au amehama watoto, ndugu na jamaa zake hawatokubali
mali hizo zirudishwe kwa CCM na kitakachotokea hapo ni ugomvi na
kupelekana mahakamani hali ambayo chama hakipo tayari kuona inatokea ”,.
Alifafanua Vuai na kuongeza kuwa CCM haitokuwa tayari kuona mali zake
zinatumiwa na watu wachache bila ya makubaliano ya kimaandishi ama
mikataba ya kisheria.
Alisisitiza
kuwa Chama hicho kitaendelea kuhakiki, kukagua na kuratibu mali zake
zote zilizopo nchini kwa lengo la kuziimarisha na endapo patajitokeza
vitendo vya udanganyifu na uvamizi vitatafutiwaufumbuzi wa kudumu na
taasisi hiyo.
Alisema
bila ya kuwepo na utaratibu maalum na endelevu wa kuhakiki mali za
chama hicho baadhi ya watu watakuwa wanajimilikisha na kujinufaisha
wenyewe huku chama kikibaki kuwa maskini.Alifahamisha
kwamba CCM itaendelea kutekeleza kwa vitendo sera zake zinazoelekeza na
kukitaka Chama kutumia rasilimali na vyanzo vyake vya mapato kukuza
uchumi wa taasisi hiyo.
Alitoa
wito kwa Wana CCM na wananchi kwa ujumla kuunga mkono juhudi za chama
hicho za kuhakikisha mali zake zinabaki salama bila ya kuhujumiwa na
watu wachache wanaojali maslahi binafsi badala ya Chama na Serikali kwa
ujumla.Wakati
huo huo Naibu Katibu wa CCM Zanzibar, alitembelea Jumba la kihistoria
la Afro-Shiraz Party (ASP) lililopo katika eneo la Kijangwani na kueleza
kwamba dhamira ya CCM ni kuhakikisha eneo hilo linaenziwa kwa kujengwa
nyumba ya kisasa zinazoendana na hadhi ya Chama.
Alifafanua
kwamba Jengo hilo lilianzishwa na Chama cha Shiraz association ambacho
baadae mwaka 1957 iliungana na Chama cha African association na kuunda
Chama kimoja kilichoitwa Afro Shiraz Party(ASP) , na hatimaye kuungana
na TANU na kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977.
“
Jengo hili lina historia kubwa ya Chama kwani lilikuwa likitumika na
viongozi mbali mbali wa chama kabla na baada ya harakati za Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964”, alisema Vuai.Aidha
amewataka viongozi wa Mkoa Mjini kuhakikisha wanaadhika historia ya
eneo hilo na kuiweka katika kumbukumbu za kudumu za chama ili ziweze
kuwanufaisha vizazi vya sasa na vijavyo.
Naibu
Katibu Mkuu huyo, aliwapongeza wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa
ujumla kwa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Mkuu wa marudio
ulioiweka madarakani CCM, na kuwasihi kufanya kazi za ujenzi wa Taifa
kwa bidii huku wakisubiri Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.
Nao
Viongozi wa Mikoa miwili kichama ikiwemo Mkoa wa Magharibi na Mkoa
Mjini kwa nyakati tofauti wameipongeza CCM kwa uamuzi wake wa kukagua
mali za chama katika maeneo tofauti ya mikoa hiyo, na kuahidi kuendelea
kuunga mkono hatua hiyo itakayosaidia Rasilimali za chama kubaki salama.
Katika
ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu huyo ametembelea maeneo mbali mbali
yakiwemo Viwanja vya Chama katika eneo la Mbweni, Nyumba ya Chama eneo
la Shangani pamoja na Jumba la kihistoria la ASP lililopo Kijangwani
Zanzibar, ambapo ziara hiyo itakuwa ni endelevu kwa upande wa Unguja na
Pemba.
No comments:
Post a Comment