Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mhe.
Dianna Melrose alipokuja Wizarani kumuaga mara baada ya kumaliza muda
wake wa uwakilishi hapa nchini. Katika mazungumzo yao Waziri Mahiga
alimpongeza Balozi Melrose kwa kuiwakilisha nchini yake vema na
kuendeleza mahusiano mazuri kati ya Tanzania na Uingereza. Kwa upande wa
Balozi Melrose, alisema anaishukuru Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano
aliokuwa anaupata kipindi chote cha uwakilishi wake.
Mkurugenzi
wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine(wa kwanza
kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Bi. Mindi Kasiga (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Mona
Mahecha nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea.
Mazungumzo yakiendelea
Wakati huo huo Mhe. Waziri Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Canada nchini.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Canada nchini, Mhe Alexandre
Leveque alipokuja Wizarani kumuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa
uwakilishi hapa nchini. Mhe. Mahiga alimpongeza na kumshukuru kwa
kuendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo
Elimu na Biashara. Pia Mhe . Alexandre Leveque alitumia fursa hiyo
kuishukuru Wizara kwa ushirikiano katika kipindi chake chote cha
uwakilishi hapa nchini.
Mkurugenzi
wa Idara ya Amerika na Ulaya Balozi Joseph Sokoine(wa kwanza kushoto),
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga (wa
kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Bi. Lilian Kimaro wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini.
Balozi Mahiga akiagana na Balozi Leveque mara baada ya kumaliza mazungumzo
.... Mazungumzo na Balozi wa Ireland hapa nchini
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt. Augustine
Mahiga akizungumza na Balozi wa Ireland nchini, Mhe. Fionnuala Gilsenan
alipokuja Wizarani kuaga mara baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi
hapa nchini. Mhe. Mahiga alimpongeza na kumshukuru kwa kuimarisha
ushirikiano kati ya Tanzania na Ireland katika sekta mbalimbali. Kwa
upande wa Mhe. Gilsenan alitumia fursa hiyo kuishukuru Wizara na
Serikali kwa ujumla kwa ushirikiano.
No comments:
Post a Comment