Na Mathias Canal, Singida
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu ametangaza rasmi siku ya
Jumatano kuwa siku ya kazi za pamoja katika majengo ya Umma katika
Vijiji vilivyopo Wilayani humo.
Tangazo
hilo amelitoa kwenye halfa iliyofanyika katika ukumbi wa Wilaya ya
Ikungi Mkoani Singida wakati anakabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa
Wilaya hiyo ambaye kwa sasa amestaafu Gishuli Charles.
Mtaturu
amesema kuwa Uongozi utachagua kama ni Shule, Zahanati au Utengenezaji
wa Barabara n.k.ambapo Wananchi wote watapaswa kushiriki kazi hiyo ili
warejeshe moyo wa kushiriki shughuli za maendeleo ambapo mkuu huyo
amesema yeye atafanya kazi ya kupita katika maeneo tofauti kuungana na
Wananchi katika kukamilisha kwa vitendo jambo hilo..
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwa ofisini mara baada ya
kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye kwa sasa
amestaafu Gishuli Charles.
Amewakumbusha
wananchi kuwa wakati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na
wenzake waliokuwa wanaanza harakati za kudai Uhuru walienda Umoja wa
Taifa wakahakikisha tunaweza kujitawala na kujisimamia wenyewe bila
mkoloni.
Mwaka
1961 tulipopata Uhuru Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alieleza sasa
tumepata uhuru tubadili malengo ya Taifa iwe ni Uhuru na Kazi aliamini
kupitia kazi tutapata maendeleo.
Awamu
ya Tano imekuja na kauli mbiu ya “HAPA KAZI TU”; kwa maana hiyo hiyo
kuhimiza Wananchi kufanya kazi na kazi ndio kipimo cha utu.
Mkuu
huyo amesema kuwa wananchi wote wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili
kuweza kuboresha maisha ya kila mmoja na familia zetu kwa ujumla.
baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye kwa sasa amestaafu Gishuli Charles.
Mkuu
huyo amesema kuwa Kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi
mwaka 2015 – 2020. Ibara ya 49 imeeleza Serikali kuongeza huduma za
Afya, kuongeza Wataalamu wa Afya kwenye Zahanati, Vituo vya Afya,
Hospitali za Wilaya n.k.
Amesema
Ilani imetambua yaliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Nne katika
Sekta ya Afya kama msingi wa kuendeleza juhudi zaidi kupiga vita
Malaria, UKIMWI, Vifo vya Mama na Mtoto n.k. Uboreshaji na upatikanaji
wa dawa na vifaa tiba.
Katika
Wilaya ya Ikungi kuna upungufu wa asilimia 62% ya Zahanati hivyo
kufanya akina Mama Wajawazito kutembea mwendo mrefu kufuata ushauri wa
kitaalamu.
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu wakikabidhiana nyaraka na
aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye kwa sasa amestaafu Gishuli Charles.
Huduma
ya kuzuia maambukizi ya VVU kwenda kwa mtoto (PMTCT) vimeongezeka ila
bado havitoshi; Vituo vya tiba vya maangalizi ya wanaoishi na VVU (CTC)
bado ni vichache sana.
Ili
kutatua changamoto ya huduma duni za afya Mtaturu ameshauri Wananchi
kuhamasishwa kujiunga kwenye Mifuko ya Bima ya Afya kama NHIF, CHF n.k.
na kusema kuwa Faida ya kujiunga na Bima ya Afya msingi wake ni kuwa
ugonjwa hauna taarifa hivyo unaweza kuugua siku hauna fedha Bima
ikakusaidia.
Katika
sekta ya upatikanaji maji safi na salama amesema kuwa Ni lengo la
Serikali kuhakikisha Wananchi wake wanapata Maji Safi na Salama kwa
kushirikiana na Wadau wa Maendeleo na Wananchi hivyo ameahidi Kuzipa
uwezo Kamati za Maji katika Vijiji ili kusimamia Miradi iliyopo iwe
endelevu ikiwemo kusoma Mapato na Matumizi kwa Wananchi kwa Mujibu wa
Sheria.
Katika
swala la Ukusanyaji wa Mapato Mtaturu amesema kuwa Changamoto
iliyopatikana kipindi kilichopita ni kuwa chini ya 80% ya lengo la
ukusanyaji mapato hivyo Kuanzia tarehe 01Julai, 2016 Serikali imeamua
sasa Halmashauri zitakusanya zenyewe mapato badala ya Wazabuni.
Miraji
Mtaruru amezungumzia pia suala la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi SURA YA
TANO YA ILANI YA UCHAGUZI MKUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI Ibara ya 56.
Imeeleza dhamira ya kuwezesha Wananchi kiuchumi kupitia Ushirika
(SACCOS& VICOBA) ikizingatiwa kupitia vikundi ndio mahali pekee
unaweza kuwapatia mitaji na kutakuwa na nidhamu ya fedha.
Hivyo
amewahimiza Maafisa Ushirika, Maendeleo ya Jamii kuendelea kuwajengea
uwezo Wananchi ili kurahisisha Serikali kushusha fedha za mitaji.
Katuika
swala la Watumishi Hewa Mtaturur amesema kuwa Pamoja na juhudi za
Serikali kuboresha masilahi ya Watumishi ila kumejitokeza uzembe mkubwa
wa watu kulipwa wasiostahili.
“Natoa
muda wa Wiki moja Mkurugenzi na timu yako mnipatie taarifa kamili
kuhusu Wafanyakazi hewa na imebainika Idara ya Elimu ndio inayoongoza
kuwa na Watumishi hewa, swali la kujiuliza Afisa Utumishi, Mratibu Elimu
Kata ambao kazi yao kila siku ni kushughulika na Kada hiyo anakuwa
hajui kama kuna watu wanalipwa wasiokuwepo kazini? Hali hii haikubaliki
na hakika tutachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kuingizia
Serikali hasara ya aina yeyote.” Amesema Mtaturu
Mkuu
huyo amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano imeamua kupitia Ilani ya
Chama Cha Mapinduzi Ibara ya 51; imefafanua namna Elimu iliyowekewa
msisitizo. Elimu ya Awali; Elimu Msingi na Sekondari hadi Chuo Kikuu
ikiwa ni pamoja na Kuboresha masilahi ya Walimu ikiwa pamoja na madai
yao ili wapate moyo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi, na Ahadi ya Elimu
bila kulipa ada Shule ya Msingi hadi Kidato cha Nne imeanza utekelezaji
mwaka huu ingawa imekutana na changamoto kwa kupata upungufu wa Madarasa
n.k.
Aidha
Pamoja na hayo bado kuna baadhi ya watoto wenye sifa za kwenda Shule
hawajaandikishwa; kimsingi ni haki ya kila mtoto kupatiwa Elimu, hivyo
wazazi wasiowapeleka Watoto Shule wanakiuka Sheria.
Mtaturu
ametoa maagizo ya Watoto wote waliofikia umri wa kwenda Shule; Maafisa
Tarafa, Watendaji Kata na Vijiji wampepe taarifa na hatua walizochukua.
“Kuhusu
upungufu wa Nyumba za Walimu, Vyumba vya Madarasa, Maabara
zisizokamilika, matundu ya vyoo, vitendea kazi n.k. ni lazima tuweke
mpango wa pamoja kuondoa changamoto hizo ili kuhakikisha Watoto waliopo
Shuleni wanapata elimu bora” Amesema Mtaturu
Wilaya
ya Ikungi ina jumla ya wakazi 272,959 na ongezeko la watu kwa mwaka ni
2.8% hivyo sasa kunakadiriwa kuwa 303,000 kwa mwaka 2015/2016 kwa mujibu
wa Sensa ya mwaka 2012
No comments:
Post a Comment