Matukio : Mhandisi Sophia Mgonja atembelea banda la shirika la Umeme (Tanesco) Saba saba - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 7 July 2016

Matukio : Mhandisi Sophia Mgonja atembelea banda la shirika la Umeme (Tanesco) Saba saba


 Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa shirika hilo katika maonesho ya 40 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam 2016 kwenye viwanja vya Biashara vya Mwalimu Nyerere  Barabara ya Kilwa  Dar es Salaam leo.
 Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya kuendeleza jotoardhi Tanzania(TGDC) wa pili kushoto akitoa maelezo kwa Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja.
 Kaimu Meneja Uhusiano Tanesco, Leila Muhaji (kushoto), akiwa na  Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja walipotembelea banda la TGDC.
 Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Sophia Mgonja (kushoto), akimsikiliza mteja aliyetembelea banda hilo.
 Mteja akisikilizwa.
 Wateja wakipata maelekezo kutoka kwa mfanyakazi wa Tanesco (kulia), jinsi ya kuunganishiwa umeme katika chumba kimoja hadi viwili.

Mtaalamu wa Tanesco akiwaonesha wananchi jinsi ya kuunganisha umeme katika nyumba za makazi

No comments:

Post a Comment