Muziki na Maisha : Rapper Lil Wayne Akimbizwa Hospitali Baada Ya Kuugua Ghafla Akiwa Kwenye Ndege - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 14 June 2016

Muziki na Maisha : Rapper Lil Wayne Akimbizwa Hospitali Baada Ya Kuugua Ghafla Akiwa Kwenye Ndege

Lil Wayne Apatwa na Kifafa na kulazimika ndege yake kutua ghafla
Lil Wayne

Na Jeff Msangi, 
Rapper Lil Wayne ambaye alikuwa safarini katika ndege binafsi ya kukodi (private jet) kutoka Milwaukee kuelekea California, amepatwa na ugonjwa wa kuanguka kifafa( epilepsy/seizure) na hivyo ndege yake kulazimika kutua kwa dharura Omaha,Nebraska ili apelekwe hospitali.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, awali ndege ilipotua Lil Wayne ambaye ameshawahi kupatwa na ugonjwa huo mara kwa mara ikiwemo mwaka 2012 na 2013 akiwa ameshapata fahamu, alikataa kupatiwa matibabu.
Hata hivyo,ndege ilipoondoka tena, alipatwa tena na hali na hivyo ikabidi safari iahirishwe na kumkimbiza CHI Health Creighton University Medical Center ambapo amelazwa.
Alipolazwa mwaka 2012 alilazimika kukaa hospitali kwa zaidi ya wiki moja akipatiwa matibabu kutokana na mashambulizi ya ugonjwa wa kifafa kumrudia mara kwa mara. Na kama ilivyokuwa mwaka 2012, Lil Wayne ambaye jina lake kamili ni Dwayne Michael Carter Jr (33),anaonekana kupatwa zaidi na ugonjwa huu anapokuwa safarini kwenye ndege na anapotumia vilevi.
Ratiba yake ya show inaonyesha kwamba anatakiwa ku-perform Jumamosi hii katika ukumbi wa Sprint Centre huko Kansas City pamoja na 2 Chainz na Tech N9ne. Haijajulikana kama ataendelea na ratiba hiyo. Ratiba ya ukumbi huo inaonyesha show bado ipo pale pale.

No comments:

Post a Comment