Matukio : Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ashiriki kampeni ya Media Car Wash mjini Dodoma - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 26 June 2016

demo-image

Matukio : Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ashiriki kampeni ya Media Car Wash mjini Dodoma

   Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson ashiriki kampeni ya Media Car Wash mjini Dodoma
index
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson akiosha gari la Mbunge wa Nanyamba, Abdallah Chikota wakati wa kampeni ya Media Car Wash ya kuchangisha fedha za kusaidia wanahabari kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kwenye Uwanja wa Jamhuri  mjini DodomaW Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson wakati wa harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini.

DSC_0003
Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja akisalimiana na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani wakati wa harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. 
DSC_0019
Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson akizungumza na baadhi ya wabunge na wageni mbalim bali kuelezea lengo la kampeni hizo asubuhi njini Dodoma. 
DSC_0026
Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani. 
DSC_0065
Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na Mkongwe wa Bongo Fleva Inspector Haroun wakiosha moja ya magari yaliofika kuoshwa kwa ajili ya harambee ya kuosha magari kupitia kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ yenye lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. 
DSC_0074
Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel (kushoto) na Mkongwe wa Bongo Fleva Inspector Haroun na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima wakiosha gari. 
DSC_0091
Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani (kulia) akimkabidhi fedha za kuoshewa gari Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel. 
DSC_0103
Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani (kushoto) wakijitolea kuosha magari kwenye kampeni hizo.


DSC_0119
Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel na mpiga picha wa magazeti ya The Guardian Ltd, Halima Kambi wakiosha moja ya gari katika kampeni hizo.
DSC_0130
Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson akishiriki zoezi la kuosha magari.
DSC_0160
Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto akishiriki zoezi la kuosha magari kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ Dodoma leo.
DSC_0163
Mbunge wa Kilolo Venance Mwamoto (kushoto) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) wakishiriki zoezi la kuosha magari kuchangisha fedha kwa ajili ya kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *