Wakazi wa Kata ya Muriet jiji la Arusha wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda. |
Mratibu wa Tasaf Jiji la Arusha,Tajiel Mahega akisoma taarifa kabla Kaya zilizotambuliwa kukabidhiwa rasmi. |
Sehemu ya Kuku wa kienyeji waliokabidhiwa wananchi kutoka Kaya masikini. |
Arusha.Mkuu wa Mkoa wa
Arusha,Daudi Felix Ntibenda ametos wito kwa wananchi wa Kata ya Murieti
kuhakikisha wanajenga Shule ya Sekondari ili kusogeza huduma hiyo kwa wanafunzi
wa maeneo hayo wanaotembea umbali mrefu kufuata shule.
Wito huo ameutoa juzi
wakati wa uzinduzi wa mradi wa ufugaji wa Kuu wa asili (Kienyeji ) na
Mbuzi wa Maziwa kwa kaya 85 za Mtaa wa
Terrat Mlimani katika Jiji la Arusha kupitia Mradi wa TASAF III
unaofadhiliwa na Umoja wa Nchi zinazozalisha Mafuta (OPEC).
Katika uzinduzi huo Ntibenda
aliwahimiza wananchi hao kutafuta eneo linalofaa kujengwa
Shule hiyo,kisha Mstahiki Meya wa Jiji kwa kushirikiana na Diwani kuitisha
harambee ya kuchangia ujenzi wa Shule ya Sekondari katika Kata hiyo.
Pia aliwasihi wananchi
kuwa makini na mradi huu wa Ufugaji ili uweze kuinua kipato na kuboresha maisha
ya wakazi wa Terrati Mlimani na maeneo mengine ambayo yametambuliwa kuwa ni
masikini.
Mtaa huu ni mojawapo
kati ya mitaa 70 ya Jiji la Arusha inayonufaika na uhawilishaji wa Fedha
kunusuru Kaya masikini ambapo kila baada ya miezi miwili hupokea jumla ya Tsh
3,182,000 kwa ajili ya kaya zilizoko kwenye mradi.
Akizungumza katika
hafla hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha,Calist Lazaro aliwawapongeza Menejimenti ya Jiji kwa
kusimamia zoezi zima la Uhawilishaji wa Fedha kwa masikini kwa kuwalenga
wananchi wale wenye kipato cha chini kama ilivyo malengo ya mradi huu.
Mwishoni mwa mwaka
2015, Halmashauri ya Jiji iliomba Fedha zaidi ya Milioni mia tatu kutoka Tasaf
kwa ajili ya utekelezaji wa miradi Tisa ambayo ni Ujenzi wa madarasa 2 Shule ya
Msingi Azimio,Ujenzi wa Bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Korona, na kwenye maeneo
yenye uhaba wa chakula .
Miradi itakayotekelezwa
ni Ujenzi wa Kivuko Mtaa wa Oloresho, upandaji wa miti na miche mtaa wa Ally
Nyanya pamoja na upandaji wa miti na miche mtaa wa Osunyai.
Pia mradi huu
haukusahau makundi maalumu kama Ushonaji eneo la Kambi ya Fisi, Ufugaji wa Kuku
wa kienyeji eneo la Moivio , Mradi wa Kuku wa kienyeji na Mbuzi Terrati Mlimani
na mradi wa ufugaji wa Kuku wa kienyeji eneo la Lolovono.
Mpaka sasa Halmashauri
imepokea jumla ya Tsh 74 milioni kwa
ajili ya kununua Kuku, Mbuzi na kutoa chakula, madawa kwa kipindi cha miezi
sita katika Mtaa wa Terrati Mlimani, Lolovono pamoja na Moivoi.
No comments:
Post a Comment