Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka
wa fedha 2016/2017 leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo akitoa ufafanuzi kuhusu wizara hiyo leo Bungeni mjini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Hamis Andrea Kigwangalla (kushoto) akiwa Bungeni
leo mjini Dodoma. Kulia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Dkt.
Ashatu Kijaji.
Baadhi
ya Wabunge wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa
Rais, Mazingira na Muungano January Makamba (hayupo pichani) alipokuwa
akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka wa
fedha 2016/2017 Bungeni mjini Dodoma.
Mashududa
walihusika katika zoezi la kuchanganya udongo wakati wa Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964, wakiwa Bungeni leo mjini Dodoma
kwa mwaliko wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na
Muungano January Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango
wao katika kuuenzi na kuulinda Muungano wa Tanzania.
wanafunzi
wa kidato cha tatu kutoka shule ya Sekondari Mnarani iliyopo jijini
Mwanza Getrude Clement akiwa Bungeni leo mjini Dodoma kwa mwaliko wa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January
Makamba ambapo Serikali imetambua na kuthamini mchango wake kwenye
utunzaji wa mazingira. Mwanafunzi huyo alihutubia viongozi mbalimbali wa
dunia kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa uliohusu mabadiliko ya tabia
nchi, uliofanyika New York Marekani.
Naibu
Spika Dkt Tulia Ackson katika picha ya pamoja
na mashuhuda waliohusika katika zoezi la kuchanganya udongo wakati wa
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili 26, 1964. Mashuhuda hao
walikuja kutembelea Bunge Mei 2, 2016.
(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Dodoma)
No comments:
Post a Comment