Sherehe
ya maadhimisho ya miaka 6 ya Chama cha Watanzania Waliosoma China kwa
kiingereza China Alumni Association of Tanzania (CAAT) imefana kwa
kiwango kikubwa.
Sherehe
hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Cardinal Laurian Rugambwa Social
Centre pembezoni mwa kanisa la Mtakatifu Peter (St Peter), Oysterbay
Ijumaa ya tarehe 20-May-2016.
Mgeni
rasmi wa sherehe hiyo alikuwa Prof Elisante Gabriel (Katibu Mkuu,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo) akimuwakilisha Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye. Wageni wengine wa
heshima walikuwa Counselor Gao Wei wa ubalozi wa China (ambaye alikuwa
anamuwakilisha balozi Dr Lu Youqing) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika La Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (Tanzania Industrial
Research Developments Organization-TIRDO) Prof Mkumbukwa Madundo Angelo
Mtambo.
HISTORIA FUPI YA CAAT
•CAAT
ni chama kilichoanzishwa mwaka 2010 ambapo mkutano mkuu wa kwanza wa
chama (General Assembly) ulifanyika Jumapili ya tarehe 14-Nov-2010
katika ukumbi wa Rombo Green View Hotel, Sinza/Ubungo, Dar-es-Salaam
(ambao hivi sasa unaitwa Rombo Hotel).
•Baada
ya hapo, sherehe za uzinduzi/ufunguzi rasmi wa chama zilifanyika
Alhamis ya tarehe 11-Aug-2011 katika ukumbi wa Karimjee, Dar-es-Salaam.
•Awamu
ya kwanza ya uongozi ya CAAT (2010-2016) iliongozwa na Eng Fred Maiga
(Mwenyekiti), Dr Haji Mwita (Makamu Mwenyekiti), Eng Mosses Swai
(Katibu) na Wajumbe: Dr Paul Peter Mhame, Dr George Oreku, Ponera Ally
Kacheuka, Eng Francis Mugisha, Gustav Sanga, Hawa Ngasongwa na Dr Uwesu
Mchepange.
•Baada
ya uchaguzi uliofanyika kwenye Mkutano Mkuu wa Jumamosi tarehe
20-Feb-2016 katika eneo la New Msasani Club viongozi wapya ni Dr Paul
Peter Mhame (Mwenyekiti), William Kaijage (Makamu Mwenyekiti), George
Oreku (Katibu Mkuu), Ponera Ally Kacheuka (Naibu Katibu Mkuu),
Johnspeter Majura (Naibu Katibu Mkuu) pamoja na Shija Boniphace Bundala
(Mweka Hazina).
Mgeni
rasmi Prof Elisante Gabriel (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo) akitoa hotuba akimuwakilisha Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye
Mwenyekiti wa Chama cha Watanzania Waliosomea China (CAAT) Dr Paul Peter Mhame akitoa hotuba.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika La Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (Tanzania
Industrial Research Developments Organization-TIRDO) Prof Mkumbukwa
Madundo Angelo Mtambo akitoa hotuba.
Mgeni
rasmi Prof Elisante Gabriel (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo) akizindua rasmi tovuti ya chama cha Watanzania
Waliosomea China (CAAT).
Mgeni rasmi Prof Elisante Gabriel (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo) akikagua maonesho ya bidhaa na huduma za
kibiashara zinazotolewa na baadhi ya watanzania waliopata kusomea China.
Picha ya pamoja kati ya mgeni rasmi, wageni waheshimiwa na viongozi wa Chama cha Watanzania Waliosomea China.
Picha ya pamoja ya watanzania waliosomea China.
Mgeni
rasmi Prof Elisante Gabriel (Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo) akikata keki ya maadhimisho ya miaka 6 ya chama cha
Watanzania Waliosomea China.
No comments:
Post a Comment