Mkurugenzi
wa Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Kilima akitoa neno la
shukrani kwa Waziri Mahiga kwa niaba ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pamoja na kuahidi kufanyia
kazi nasaha zilizotolewa, Balozi Kilima alimpongeza Waziri Mahiga kwa
kuwa kiongozi bora na wa mfano wa kuigwa na Watumishi wote katika
utendaji wa kazi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akimkaribisha Waziri wa Wizara
hiyo Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga kwenye mkutano wa Baraza la
Wafanyakazi uliofanyika Mei 27, Jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere.
Mhe.
Waziri Mahiga akiwahutubia watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza
la Wafanyakazi wa Wizara. Katika hotuba yake aliwaasa watumishi kuwa
waadilifu, kufanyanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuhakikisha shughuli
za kidiplomasia zinafanyika kwa tija ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Sera
ya Mambo ya Nje inatekelezwa na kuifanya Tanzania kuendelea kupaa
katika medani za kimataifa.
Balozi
Ramadhan Muombwa Mwinyi akitoa taarifa ya utangulizi ya mkutano kwa
Mhe. Waziri, Viongozi wa TUGHE-Taifa pamoja na wafanyakazi waliohudhuria
Mkutano huo hawapo pichani. Pia alitumia fursa hiyo kumkaribisha Mhe.
Waziri ili aweze kufanya ufunguzi wa Mkutano ambapo tukio hilo
liliambatana na utoaji wa zawadi za wafanyakazi bora wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Sehemu
ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba
Sehemu
nyingine ya Wakurugenzi, Wakuu wa Vitengo na Watumishi wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba.
Mjumbe
kutoka TUGHE-Taifa, Bw. Arcado Nchinga pia alizungumza na Watumishi wa
Wizara ambapo aliwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa juhudi ikiwa ni
pamoja na kuhakikisha wanaiwakilisha nchi vizuri katika mataifa mengine.
Mkurugenzi
wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Bw. Nigel Msangi akitoa
taarifa ya wafanyakazi bora wa Wizara wa mwaka 2015/2016 kwa Waziri
Mahiga ambao walitunukiwa zawadi katika mkutano huo.
Afisa
Habari katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Bw. Ally Kondo ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari wa iliyokuwa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Pichani akipongezwa
na Mhe. Waziri Mahiga.
Afisa
TEHAMA katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Bw.Salum M. Nalolah ndiye aliyeibuka Mfanyakazi Bora na Hodari wa
iliyokuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Pichani akipongezwa
na Mhe. Waziri Mahiga.
Picha ya pamoja ya Mhe. Waziri na Wafanyakazi bora wa Idara zote za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Picha
ya pamoja Mhe. Waziri Mahiga na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment