Sehemu
ya Wakimbiaji wa Mbio za Mwenge, wakiwa tayari kuupokea Mwenge huo
ulipowasili kwenye Kituo uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na
matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, kilichopo eneo
la Ukuni, Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Mei 19, 2016. Zaidi ya vijana
40 waliokuwa wameathiriwa na matumizi ya Madawa ya kulevwa wanalelewa
katika kituo hicho.Picha zote na Othman Michuzi - MMG.
Mmoja
wa wakimbiza Mwenge huo, akiongoza mbio hizo wakati Mwenge wa Uhuru
ulipokuwa ukiwasili kwenye Kituo uangaliazi maalum kwa watu
walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober
House, kilichopo eneo la Ukuni, Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani Mei 19, 2016.
Mwenge umehifadhiwa kwenye sehemu yake.
Mmiliki
wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya
madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji, akitoa
taarifa fupi ya kituo hicho kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa,
George Jackson Mbijima (hayupo pichani) wakati Mwenge huo ulipotembelea
kituo hicho Mei 19, 2016.
Mmiliki
wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya
madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji (kulia)
akikikabidhi taarifa hiyo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa,
George Jackson Mbijima, mara baada ya kuisoma.
Mmoja
wa Vijana waliokuwa wameathiriwa na Madawa ya Kulevya ambaye sasa
amerudi katika hali yake ya kawaida baada ya kupatiwa tiba aliefahamika
kwa jina la Abdullatif, akisoma ngonjera aliyoiandaa mwenyewe yenye
ujumbe wa kuwataka vijana wengine kuachana kabisa na matumizi ya madawa
ya kulevya, kwani yanaathari kubwa kwao.
Abdullatif akimtabithi Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima ngonjera yake hiyo.
Sehemu vijana waliokuwa wameathiriwa na matumizi ya madawa ya kulevya wakifatilia hotuba mbali mbali zilizokuwa zikitolewa.
Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanaga akizungumza machache wakati wa
halfa hiyo ya Mwenge kutembelea katika Kituo cha Bagamoyo Sober House.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima akitoa hotuba yake
ambapo aliwataka vijana hao walioamua kuachana na matumizi ya madawa ya
kulevya na kurudi katika shughuli za ujenzi wa taifa, kwani vijana ni
nguvu kazi ya taifa.
Picha ya pamoja na baadhi ya vijana hao.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, George Jackson Mbijima (kushoto) akimkabidhi Mwenge, Mmiliki
wa Kituo cha uangaliazi maalum kwa watu walioathirika na matumizi ya
madawa ya kulevywa cha Bagamoyo Sober House, Al Karim Bhanji, wakati wa
hafla fupi ya Mwenge huo ulipotembelea kituo chake hicho. Kulia ni Mkuu
wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Mwanaga.
No comments:
Post a Comment