Matukio : Mwanafunzi Mbaroni Kwa Kumtukana Rais Wa Zanzibar Dkt.shein Pamoja Na Mkuu Wa Majeshi Mwamunyage. - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


22 May 2016

Matukio : Mwanafunzi Mbaroni Kwa Kumtukana Rais Wa Zanzibar Dkt.shein Pamoja Na Mkuu Wa Majeshi Mwamunyage.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo.


Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia mwanafunzi wa Mwaka wa
tatu wa chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru aliyejulikana kwa jina la
Harold Mmbando (23) mkazi wa Arusha kwa kosa la kutoa taarifa za
uchochezi dhidi ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na Mkuu
wa majeshi Davis Mwamunyange pamoja na kusambaza ujumbe wa
maneno makali juu ya viongozi hao.

Akiongelea tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles
Mkumbo alisema kuwa tukio hilo lilitokea May 17 mwaka huu majira ya
saa 09:00 asubuhi .

Alisema kuwa mwanafunzi huyo alitoa taarifa za uchochezi kuhusu mkuu
wa majeshi ambapo alimtaka mkuu huyo wa majeshi kupindua nchi na
kusema kuwa haiwezekani viongozi wote wawe nje ya nchi huku akuna
kiongozi aliyepewa mamlaka ya kukikaimu kiti.

“Mtuhumiwa huyo aliandika maneno haya ,Mwamunyange pindua nchi
haiwezekani wote wawe nje halafu hakuna aliyepewa mamlaka ya
kukalia kile kiti, hayo ndio maneno aliyoyasema mtumiwa huyo “alisema
Mkumbo.

Aidha aliongeza kuwa mbali na maneno hayo pia mtumiwa huyo
alisambaza ujumbe mwingine wenye maneno yafuatayo, ”Dr Shein
akiuawa kama Karume sitashangaa wala kustuka naomba mungu
mauaji ya kisiasa yaliyotokea Zanzibar yawe kwa viongozi wa kisasa
hasa watawala na sio wananchi wa kawaida hayo ndio maneno
aliyoyaandika mtuhumiwa huyo kupitia mitandao ya kijamii kama
facebook."

Mkumbo alisema kuwa mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani pindi
tu upelelezi utakapo kamilika,huku akitoa rai kwa watu wote wanaotumia
mitandao ya kijamii kutumia mitandao hiyo ya kijamii pasipo kukiuka
sheria na taratiu za kisheria .

Alitumia muda huo pia kutoa onyo kali kwa yoyote atakaye bainika
anatumia mitandao vibaya na kusema kuwa atachukuliwa hatua kali za
kisheria dhidi yake.

Wakati hayo yakiendelea mshtakiwa wa kesi ya kumtukana Rais wa
Jamuhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli Isaac Emily
(40), mkazi wa Olasiti jiji hapa inatarajiwa kuanza kusikilizwa mfululizo
kuanzia Juni 5 mwaka huu katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad