Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto),
Flaviana Matata na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na
Muungano January Makamba wakiweka shada la maua kwenye kaburi la pamoja
ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya kuzama kwa
meli ya MV. Bukoba.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoaja na
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January
Makamba wakijiandaa kuwasha mishumaa.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto)
akiweka mshumaa kwenye kaburi pamoja na Flaviana Matata kwenye
maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa MV. Bukoba ambapo mamia ya watu
walipoteza maisha.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kulia)
akimsikiliza Flaviana Matata muda mfupi kabla ya kupiga picha ya pamoja
za kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa meli ya MV.
Bukoba.
Picha ya Pamoja.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza
wakati wa kuangalia mazoezi ya uokoaji majini yaliyofanywa na vijana 50
waliohitimu mafunzo ya uokoaji yaliyodhaminiwa na Flaviana Matata
Foundation pamoja na UTT wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20
tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba yaliyofanyika mjini Mwanza ambapo
mamia ya watu walifariki akiwemo mama mzazi na binamu wa Flaviana
Matata.
Sehemu
ya waliofuzu mafunzo ya uokoaji wakionyesha namna ya kuokoa watu majini
wakishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Nnauye, Mhe. January Makamba Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe.
Stanslaus Mabula na Flaviana Matata
Sehemu
ya makaburi ya pamoja ya waliofariki kwenye ajali ya MV. Bukoba mwaka
1996 ambapo leo imetimia miaka 20 tangia ajali hiyo imetokea.
Viongozi wa Dini walioshiriki kwenye kutoa ibada maalum ya kumbukumbu ya miaka 20 tangia kutokea kwa ajali ya MV. Bukoba.
Sheikh
Hassan Kabeke akiongoza dua wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya
miaka 20 ya ajali ya MV. Bukoba ambapo mamia ya watanzania walifariki
dunia.
Flaviana
Matata (kushoto) akiwa amejiinamia kwa huzuni wa kumbukumbu ya ajali ya
MV.Bukoba ambapo alipoteza Mama Mzazi pamoja na Binamu, katikati ni
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Kepteni Winton Mwasa na
kulia ni Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
Mchungaji
Obadi Ruralila wa KKT akiongoza ibada ya kuwaombea marehemu kwenye
kumbukumbu ya miaka 20 tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba ambapo mamia
ya wakazi wa jiji la Mwanza wakiongozwa na Flaviana Matata walijitokeza
kwenye makaburi ya pamoja ya Igoma mjini Mwanza.
Shemasi
John Kasembo wa Parokia ya Ilemelea akitoa neno la mungu wakati wa
kilele cha kumbukumbu ya miaka 20 tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
Kaimu
Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Kepteni Winton Mwasa
akizungumza machache juu ya uboreshaji wa elimu ya uokoaji waliyoitoa
kwa kushirikiana na Flaviana Matata Foundation pamoja na UTT ambapo watu
50 walihitimu mafunzo ya kuokoa majini.
Flaviana
Matata akizungumza wakati wa kumbukumbu ya miaka 20 ya ajali ya kuzama
kwa Meli ya MV Bukoba ambapo alipoteza Mama Mzazi pamoja na Binamu yake.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya jali ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauyeakizungimza
wakati wa maadhimisho yamiaka 20 ya kumbukumbu ya ajali ya MV. Bukoba
ambapo alisema imefika wakati elimu uokoaji itolewe kwa vijana wadogo
ili wawe na uelewa mkubwa wa kukabiliana na matatizo yanapotokea.
Sehemu ya wakazi wa jiji la Mwanza ambao walipoteza ndugu , jamaa na marafiki
No comments:
Post a Comment