Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akizungumza katika kikao hicho
kilicho fanyika ofisi ya kata ya Kahe ,kulia kwake ni Mkurugenzi wa
Idara ya Maafa nchini ,Brigedia Jenerali,Mbazi Msuya,kushoto ni
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila.
Diwani wa kata ya Kahe ,Rodrick Mmanyi akizungumza baada ya Mkurugenzi
wa Idara ya Maafa nchini,Brigedia Jenerali ,Mbazi Msuya kutembelea kata
hiyo kutizama athari zilizotokana na mafuriko.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Kahe wakiwa katika kikao na ujumbe wa
Mbunge wa jimbo la Vunjo uliofika katika kata hiyo kwa ajili ya kutoa
msaada wa chakula.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila
akizungumza na kutoa pole kwa wakazi wa kata ya Kahe waliofikwa na maafa
yaliyotokana na mafuriko.
Mbunge
wa Viti maalum Chadema mkoa wa Kilimanjaro,Lucy Owenya akitoa salamau
za pole kwa wakazi wa kata za Mabogini na Kahe walioathirika na mafuriko
yaliyotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha.
Sehemu ya Msaada uliotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na Mbunge wa jimbo la Vunjo ,James Mbatia.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Moshi,Michael Kilawila
akikabidhi mfuko wa Unga kwa baadhi ya wazee katika kata ya Kahe
walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mbunge wa jimbo la Vunjo,James Mbatia akikabidhi Chumvi kwa baadhi ya wazee walioathirika na mafuriko .
Wananchi katika kata ya Kahe wakifurahia pamoja na Wabunge James Mbatia
na Lucy Owenya msaada uliotolewa kwa ajili ya kusaidia wananchi
walioathirika na mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
No comments:
Post a Comment