Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (aliyesimama) akiwasilimia wakulima wadogo zaidi ya 340 (hawapo pichani) wa mkoa wa Morogoro wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe.
Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe (aliyesimama) akiwasilimia
wakulima wadogo zaidi ya 340 (hawapo pichani) wa mkoa wa Morogoro wakati
warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika
katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. Kushoto
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal.
Mkurugenzi
wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (Kulia) akiwasilisha
Mada ya Utambulisho wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo kuhusu Huduma
zitolewazo na Benki, Mpango shirikishi wa Kumsaidia Mkulima Mdogo kupata
mkopo na utalaam wa kilimo cha kisasa kwa kuwashirikisha wadau wakuu wa
Kilimo katika kumkwamua mkulima mdogo wakati warsha ya wakulima wadogo
zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe (Wapili kushoto) akizungumza
na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert Paschal (Wapili
kulia) wakati warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro
iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya
Kilombero.
Mkuu
wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe akiwa katika picha ya pamoja
na baadhi ya wakulima wadogo waliohudhuria warsha ya wakulima wadogo
zaidi ya 340 wa Mkoa wa morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira
Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) yatoa mkopo wa 890 Milioni kwa
wakulima wa zao la mpunga wanaojishughulisha kilimo cha umwagiliaji
katika Kijiji cha Mkula wilayani Kilombero ili kuongeza tija na
uzalishaji wa zao la mpunga.
Hayo
yaliwekwa bayana na Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Robert
Paschal wakati wa warsha ya wakulima wadogo zaidi ya 340 wa Mkoa wa
morogoro iliyofanyika katika Ukumbi wa Mazingira Halmashauri ya Wilaya
ya Kilombero.
Bw.
Paschal alisema lengo la mkopo huo unaowanufaisha zaidi ya wakulima 350
ni kuongeza tija na uzalishaji wa mpunga ili Kusaidia upatikanaji wa
utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania na
kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu
kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza
umaskini.
“Mkopo
huu na mengine tunayotoa imelenga kuongeza tija na uzalishaji katika
kilimo ili kusaidia kukabiliana na mapungufu hayo na kuhuisha
upatikanaji wa mikopo katika sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi katika
kilimo nchini,” alisema Bw. Paschal.
Kwa
mujibu wa Bw. Paschal mkopo huo utasaidia shughuli mbalimbali za
utayarishaji wa mashamba, kupima ubora wa udongo na virutubisho
vinavyohitajika kwenye uzalishaji wa mpunga pamoja na kuwezesha
upatikanaji wa pembejeo za kilimo zikiwemo mbegu bora, mbolea na madawa.
Mkurugenzi
huyo aliongeza kuwa Benki imetoa mkopo kwa ajili ya uwekezaji kwenye
ujenzi viwanda vya kusindika mazao, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa
mitambo ya usindikaji wa mpunga ili kuongeza thamani wa zao hilo.
“Tunaamini
mkopo huu utachagiza kuongezeka kwa upatikanaji wa chakula na Pato la
Taifa kutokana kuongezeka kwa tija na uzalishaji hivyo kuwa chachu ya
ongezeko la thamani, ukuaji wa viwanda vya mazao ya kilimo hivyo
kuchangia kuongezeka kwa ajira nchini,” aliongeza.
Akizungumzia
mikakati ya TADB kwa sasa, Bw. Paschal alisema Benki imejipanga kutoa
mikopo ya Muda Mfupi, Mikopo ya Muda wa Kati na Mikopo ya Muda Mrefu kwa
kutumia njia mbalimbali. Mbinu hizo zinajumuisha pamoja na mambo
mengine; mikopo ya moja kwa moja kwa vikundi vya wakulima wadogo wadogo;
kutoa mikopo kwa njia ya marejesho taasisi zinazokopesha; utoaji wa
mikopo kwa pamoja na kushirikiana na taasisi/benki zingine; pamoja na
mikopo ya miundombinu inayolenga kupunguza mapengo ya upatikanaji wa
fedha katika minyororo ya ongezeko la thamani ya kipaumbele.
“Kwa
kuanzia, TADB imelenga uwekezaji katika maeneo nane (8) ya minyororo ya
uongezaji wa thamani ambayo ni: nafaka, kilimo cha mboga mboga, kilimo
cha bidhaa za viwanda, mbegu za mafuta, ufugaji wa ng’ombe, ufugaji
kuku, ufugaji wa samaki na bidhaa za misitu. Benki pia inajitahidi
kusimamia fedha kutoka kwa wafadhili wengine ambazo zimeelekzwa kwenye
kuendeleza kilimo,” alisema.
Warsha
hiyo ilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Mhe. Lephy Gembe
ambaye alitoa rai kwa Wakulima wote waliopata fursa ya kuhudhuria warsha
hiyo kujipanga katika kuchangamkia fursa za mikopo inayotolewa na
TADB. Mhe. Gembe zingatia mada zilizowasilishwa ili waweze kunufaika na
Benki hii na shughuli zinazotolewa na Taasisi zingine za serikali
“Nawasihi
mrudishe mikopo mtakayopewa kwa wakati ili wakulima wengine waweze
kunufaika zaidi na Benki hii na vile vile kuwezesha Benki kutoa huduma
kwenye maeneo mengine ya Tanzania,” alisema.
No comments:
Post a Comment