Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo leo imetangaza rasmi kumfungia msanii wa bongo fleva Snura kujihusisha na masuala ya sanaa. Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Zawadi Msalla ameongea na waandishi wa habari na kuthibitisha taarifa hizi.
Wimbo huu wa Chura umefungiwa kutochezwa kwenye redio na TV nchini. Taarifa hiyo imetolewa na wizara hiyo kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wake wa mikutano wizarani hapo Dar es salaam.
Kitengo cha mawasiliano wa wizara hiyo ,Zawadi Msalla, pia imewaonya watu kutoisambaza wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo whatsApp, amedai kwa wale watakaokiuka agizo hilo watashtakiwa kutumia sheria ya makosa ya mtandao.
No comments:
Post a Comment