Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na
makampuni wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(Kushoto
aliyekaa)na Meneja mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad
Khuller(kulia)wakisaini mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya wateja wa
KLM kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma ya M-Pesa,Mkataba
huo ulisainiwa jijini Dar es Salaam leo,Anaeshuhudia katikati ni
Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa Vodacom
Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit.
Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa Vodacom
Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit(katikati)akishuhudia
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na
makampuni wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(Kushoto)na
Meneja mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad Khuller
wakibadilishana mikataba baada ya kuisaini kwa ajili ya wateja wa
KLM kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma ya M-Pesa,Hafla
hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na
makampuni wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(Kushoto)na
Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad
Khuller(kulia)wakielekeza jinsi ya kukata tiketi kupitia huduma ya M-
PESA na Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa Vodacom
Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit(katikati) wakati wa hafla
ya kusainiana mkataba kwa ajili ya wateja wa KLM kulipia tiketi zao
za kusafiri kupitia huduma hiyo,Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam leo.
Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la KLM nchini,Sharad
Khuller(kulia)akimsisitiza jambo Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha
huduma za kibiashara na makampuni wa Vodacom
Tanzania,Gregory Verbond,baada ya kusainiana mkataba kwa ajili
ya wateja wa KLM kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia huduma ya M-
Pesa,Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwa kwenye
picha ya pamoja na Kaimu Ofisa Mkuu wa kitengo cha Kifedha wa
Vodacom Tanzania,(M-Commerce),Sitoyo Lopokoiyit(kushoto) Ofisa
Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za kibiashara na
makampuni wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond(wanne toka
kushoto)pamoja na Meneja Mkuu wa Shirika la Ndege la KLM
nchini,Sharad Khuller(watano toka kushoto) wakati wa hafla ya
kusainiana mkataba kwa ajili ya wateja wa KLM kulipia tiketi zao za
kusafiri kupitia huduma ya M-PESA,Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es
Salaam leo.
Wateja
wa Shirika la ndege la Uholanzi la KLM watakaokuwa wanatumia usafiri wa
anga kuanzia sasa wataweza kulipia tiketi zao za kusafiri kupitia
huduma ya M-Pesa,Hiyo imekuja baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya
kutoa huduma hiyo kwa Kampuni hiyo na Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania leo.Huduma hii imekuwa inatumiwa na makampuni mbalimbali
kupokea malipo na kuwarahisishia wananchi maisha.
Wateja
wa shirika la KLM pia sasa wataweza kulipia huduma mbalimbali kupitia
M-Pesa badala ya kupoteza muda kutembelea ofisi za shirika hilo na
mawakala wake baadhi ya huduma hizo zikiwa ni kununua tiketi za
safari,kulipia mizigo ya ziada,malipo ya kuahirisha safari.
Akiongea
kuhusu ushirikiano huu Ofisa Mtendaji Mkuu wa kitengo cha huduma za
kibiashara na makampuni wa Vodacom Tanzania,Gregory Verbond,alisema
“Tunayo furaha kufanya kazi na shirika la KLM ambapo sasa wateja wetu
maisha yao yamezidi kurahisishwa sasa wanaweza kupata huduma za shirika
hili kupitia simu zao za mkononi kwa kufanya malipo kwa M-Pesa”.
Verbond
aliongeza kuwa mtandao wa M-Pesa hivi sasa unatumiwa na taasisi na
makampuni mbalimbali ya serikali na binafsi katika kurahisisha kupokea
malipo kwa urahisi kutoka kwa wateja wao na imethibitika kuwa njia
inayorahisisha maisha,kuokoa muda na ni salama.
Aliyataja
baadhi ya mashirika ya ndege ambayo kwa sasa wateja wake wanafanya
malipo kupitia huduma hii kuwa ni Qatar Airways, Precision Air, Kenya
Airways, Air Tanzania, Fast Jet, Eagle Air na Auric Air.
Kwa
upande wake Meneja wa Shirika la KLM nchini,Sharad Khuller alisema kuwa
wamejiunga na huduma ya M-Pesa kutokana na maombi ya wateja wake
katika kuwarahishia maisha kwa kulipia huduma wanazohitaji hususani
kununua tiketi za safari za kwenda nchi mbalimbali duniani,Huduma kwa
wateja kwa kampuni yetu ni kitu muhimu sana kwa KLM.
Ushirikiano
huu na Vodacom Tanzania kupitia huduma ya M-PESA ni njia muhimu sana
kwa kutoa huduma zilizo bora kwa wateja wetu ni huduma inayowafanya
wateja wawe huru kwa kulipia tiketi zao kwa haraka na bila
usumbufu,alisema Khuller
Kupata
huduma hii anachopaswa kufanya mteja ni kupiga namba*150* 00#,ambapo
kwenye menu ya simu yake atachagua huduma namba 4 inayoelekeza kulipa
kwa M-Pesa,baadaye atachagua huduma namba 3,kuchagua aina ya biashara ni
namba 9,kisha atachagua namba 3 inayoonyesha huduma za usafiri na
mwisho atachagua KLM
No comments:
Post a Comment